30/06/2026
Kutoka ❤️ ya Pwani ya Uswahili hadi ❤️ ya Ufaransa.
Mwezi huu wa Julai, Swahili Fashion Week inaleta fahari, uzuri na utajiri wa utamaduni wa Kiswahili, ubunifu wa Waafrika na ustadi wa hali ya juu katika jiji la Paris, mojawapo ya miji mikuu ya mitindo duniani.
Ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Kiswahili 2026, maonesho haya yanaitumia mitindo k**a daraja la kuunganisha tamaduni, kuimarisha mahusiano kati ya mataifa na kuutangaza urithi wa Kiswahili kwa ulimwengu.
Haya si maonesho ya mitindo pekee. Ni jukwaa la kuenzi utambulisho wa Kiswahili, kuhamasisha ubunifu wa Kiafrika na kufungua milango ya fursa mpya kwa wabunifu wetu katika soko la kimataifa.
Kila u*i unasimulia historia.
Kila vazi linatunza urithi.
Kila hatua kwenye jukwaa la maonesho huunganisha tamaduni.
Karibu tusherehekee pamoja uzuri, utofauti na ubunifu wa mitindo ya Kiswahili, huku tukiipeperusha bendera ya ubunifu wa Afrika duniani.
Paris, Ufaransa🇫🇷
4–7 Julai 2026
Kuadhimisha Utamaduni wa Kiswahili.
Kuunganisha Dunia Kupitia Utamaduni.
Kujenga Mustakabali Kupitia Mitindo.
Nyimbo