AKILI's Mendy Product.

AKILI's Mendy Product. There is only one way to happiness and that is to cease worrying about things which are beyond the power of our will.-

17/05/2024
Tupo online
11/01/2024

Tupo online

MKOROSHO NDIO DAWA NZURI YA KUZUIA SUMU YA NYOKA.Kuna nyoka wengi wenye sumu kali ambayo huua ndani ya masaa machacheIki...
03/10/2022

MKOROSHO NDIO DAWA NZURI YA KUZUIA SUMU YA NYOKA.

Kuna nyoka wengi wenye sumu kali ambayo huua ndani ya masaa machache

Ikiwa wewe ni mwathirika wa kuumwa na nyoka au sumu, tafuta tu mti wa mkorosho, tumia kata yako kupata magome ya mkorosho, na kutafuna magome ya mti huo.

Unapotafuna, umeze juisi, usimeze makapi. Itapunguza kila dutu yenye sumu kutoka kwa nyoka hata ikiwa ni kuumwa na nyoka aina ya Black mamba.

Gome la mkorosho linafaa sana na lina nguvu ya kuharibu sumu ya nyoka.

Unaweza kuweka gome kwa dharura yoyote, hata k**a ni kavu, loweka tu kwenye maji.
Hai haribiki, inaweza kuwekwa kwa miaka mingi bila kuharibika

Mungu ametubariki kwa mitishamba mingi sana lakini wengi hawaijui..

JINSI YA KITENGENEZA PEANUT BUTTER AU KARANGA ZA KUSAGA NYUMBANI    MahitajiBlender KarangaMafuta ya kupikia ya majiChum...
10/07/2022

JINSI YA KITENGENEZA PEANUT BUTTER AU KARANGA ZA KUSAGA NYUMBANI
Mahitaji
Blender
Karanga
Mafuta ya kupikia ya maji
Chumvi
Asali
Matayarisho
Safisha karanga zako kisha kaanga kwa moto mdogo ziive mpaka ndani harafu acha zipoe na tolea maganda ukimaliza andaa blender kule kidogo cha vitu vikavu mimina karanga kiasi usijaze weka mafuta ya kula ili kulainisha kusagika vizur na kiulaini, weka chumvi kidogo na asali anza kusaga ukiona vimelainika toa weka kwenye chombo safi chenye mfuniko na inakuwa tayar kwa matumizi.
Zinakaa muda mrefu kikubwa jitahidi kuwa unatumia kijiko kisafi na kikavu wakat wa kuchota

Baba kabla hajafa alimwambia mwanae "hapa nina saa niliyopewa na babu yako ina miaka zaidi ya mia mbili,nataka nikuzawad...
26/11/2021

Baba kabla hajafa alimwambia mwanae "hapa nina saa niliyopewa na babu yako ina miaka zaidi ya mia mbili,nataka nikuzawadie.Lakini kabla sijakupa nenda kwa sonara uone k**a watainunua kwa shilingi ngapi?"

Kijana akaenda na kumrudia babaake na kumwambia kuwa wamesema watainunua kwa shilingi elfu kumi na tano kwa sababu imezeeka sana.

Babaake akamwambia tena aende kwenye maduka ya vyuma chakavu,Alipoenda aliambiwa kuwa watainunua kwa shilingi elfu moja.

Baada ya hapo baba alimwambia aende tena kwenye jumba la makumbusho aone watainunua kwa shilingi ngapi.

Alipoenda wao wakamwambia watainunua kwa shilingi milioni kumi na tano,kwa sababu walikuwa wanatafuta sana vitu vya kale k**a hivyo.

Baada ya hapo baba alimwambia mwanae nilitaka tu ujue thamani ya kitu kikiwa sehemu yake sahihi.

"Mwanangu unaweza ukaenda mahali watu wasikupe hashima yako na wasikuthamini kabisa.

Usije umia kwa sababu hawajui thamani yako ukiona hivyo! Toka mahala hapo tambua hapo sio mahali sahihi kwako tafuta mahali pengine sahihi ambapo watatambua thamani yako.

C & P from Buyegu Shilatu

Mlipokuwa mnazungumza kuhusu tiba za kiafrika, nikamkumbuka bwana mmoja wa kuitwa Imhotep._________Leo hii ukiuliza nani...
20/06/2021

Mlipokuwa mnazungumza kuhusu tiba za kiafrika, nikamkumbuka bwana mmoja wa kuitwa Imhotep.
_________

Leo hii ukiuliza nani baba wa tiba duniani 'father of medicine' utaambiwa ni Hippocrates kutoka ugiriki anayeaminika kuwa ndiye mwanzilishi wa sayansi ya tiba. Hippocrates alizaliwa na kupata kuishi miaka ya 460BC huko Kos, Ugiriki akifundisha na kuandika vitabu vingi kuhusiana na mambo ya tiba. Inaelezwa aliweza kuandika vitabu zaidi ya 60 ikiwemo kile cha "Hippocrates Oath" kinachoelezea kanuni na misingi ya maadili ya kazi za kitabibu. Kitabu hiko ndio chanzo wa kuwepo kwa kiapo cha madaktari na manesi.

Lakini, pamoja na Hippocrates kuitwa 'father of medicine', kuna mtu mwingine wa kuitwa Imhotep, mzaliwa wa Kemet au wengine wakiita Misri ya Kale. Huyu alikuwa mtaalamu wa mambo ya tiba pale Kemet akifundisha watu namna ya kutibu magonjwa na majeraha mbalimbali kwa kutumia vitu asili. Kuna wanasayansi wanasema kuwa Imhotep ndiye anayestahili kuitwa 'father of medicine' na sio Hippocrates. Hiyo ni kutokana na kugundulika kwa nyaraka iliyoandikwa miaka ya ~2500BC ikielezea maswala ya tiba. Hiyo inatoa tafsiri kwamba miaka 2000 kabla ya kuzaliwa Hippocrates, kulikuwa na nyaraka inazoelezea matibabu na magonjwa mbalimbali. Nyaraka hiyo iliyopewa jina la "Edwin Smith Papyrus" inasemekana iliandikwa na Imhotep.

Nyaraka hiyo iliyopatikana mwaka 1862, ilituthibitishia kwamba wamisri wa kale walikuwa wakitibu majeraha kwa kutumia asali na utomvu wa miti. Pia mafuta ya mnyonyo na baadhi ya matunda k**a vile 'mitini' (figs) yalikuwa ni dawa kwa maradhi mbalimbali ikiwemo maumivu ya mitupa. Mbogamboga k**a figili zilitumika kutibu maumivu ya viungo vya mwili. Majani ya Acacia nayo yalionekana kutibu kikohozi na hadi leo inatumika. Hayo yote yalielezwa na Imhotep kwenye maandiko yake. Imhotep, hakuwa tu mtaalamu wa tiba, bali alikuwa mtawala, katika serikali ya farao Djoser aliyetawala kuanzia mwaka 2960BC. Imhotep alikuwa mshauri wa farao, na kubwa kuliko vyote alikuwa ni msanifu majengo. Yeye ndiye aliyesanifu ujenzi wa piramidi ya kwanza nchini Misri iliyojulikana k**a piramidi ya ngazi 'step pyramid' iliyopo saqqara.

Imhotep alifariki miaka ya ~2950BC. Na kutokana na utaalamu wake katika maswala ya tiba, mwaka 525BC, wamisri na wagiriki walianza kumuabudu k**a mungu wa tiba.

_________

Ahsante.

12/02/2021

ONGEZA KINGA YA MWILI NA ONDOA HOFU MOYONI ,WAKO KWA JUICE TAMU INAYOTUMIWA NA WATU WOTE

*Hii juisi ina mchanganyiko wa vitu vifuatavyo*

1. Vitunguu swaumu 2
2. Vitunguu maji 4
3. Tangawizi kubwa 2
4. Limau kubwa 5
5. Mdalasini ya Unga kijiko kidogo cha chai kimoja
6. Asali vijiko vikubwa 10
7. Maji lita moja na nusu hivi

Glasi moja kwa siku inatosha

Watoto kuanzia miaka miwili mpaka miaka 10 nusu Glasi kwa siku inatosha

*Menya vitunguu maji na uvikate vipande vidogo vidogo

*Safisha vizuri na maji tangawizi kisha zikate vipande vidogo vidogo

*Viachanishe vitunguu swaumu ili upate punje zake, usimenye hizo punje

👉Kwenye blenda weka vitunguu swaumu, vitunguu maji, tangawizi na maji kidogo. Saga hivi vyote kwa pamoja. Saga mpaka visagike vizuri kabisa. K**a blenda yako ni ndogo unaweza kusaga huo mchanganyiko kidogo kidogo mara mbili au hata 3

👉Ukimaliza kusaga hivi mimina kwenye chombo kingine na uchuje kupata juisi, taka taka zake zitupe

👉Kwenye hiyo juisi uliyochuja kamulia limau 5 moja baada ya nyingine, usiweke mbegu za limau humu, ni maji maji ya limau tu

>Kwenye hiyo juisi baada ya kukamulia limau ongeza asali vijiko 10, mdalasini ya Unga kijiko kidogo cha chai kimoja na maji yote yaliyobaki (katika ile lita 1 na nusu)

*Koroga vizuri hii juisi yako mpaka iwe kitu kimoja

👉Isiwe nzito sana wala nyepesi sana

🤝Kunywa Glasi moja (ml 250) kutwa mara baada ya chakula cha mchana au cha usiku

🤝Glasi moja mara moja kwa siku. Unaweza pia kunywa kila baada ya siku moja na siyo kila siku

🤝Watoto kuanzia miaka miwili mpaka miaka 10 nusu Glasi kwa siku kila siku au kila baada ya siku moja

😝Ukiona kichwa kinauma sana siku mbili au tatu baada ya kuwa umeanza kunywa juisi hii utatakiwa uache kunywa kwa siku mbili tatu hivi kichwa kikitulia endelea kutumia juisi

😝Mama wajawazito chini ya miezi minne wasitumie

😴Wenye vidonda vya tumbo pia wenye kisukari wanaweza kutumia juisi hii

K**a unahitaji ambayo tayari imeandaliwa na mimi, tuwasiliane inbox nauza kuanzia lita 5 kwa TSh 25000

👏Mpaka siku 3 hata 4 hivi inaweza kubaki salama bila kuhitaji friji

🤛Kwa Maelezo na msaada zaidi>

Pokea dondoo na makala mbalimbali kuhusu afya hususani zinazohusu tiba asili kupitia page yangu hii kikubwa like na ushee zaidi

Karibu

SHARE ujumbe huu na wote uwapendao

JE NI KWELI KUWA TAJIRI NDIYO KUJAWA NA FURAHA?Siku moja bilionea Femi Otedola katika mahojiano maalum kwa njia ya simu ...
05/12/2020

JE NI KWELI KUWA TAJIRI NDIYO KUJAWA NA FURAHA?

Siku moja bilionea Femi Otedola katika mahojiano maalum kwa njia ya simu aliulizwa na mwandishi wa habari: "Mheshimiwa, unaweza kukumbuka ni jambo gani lililokufanya kuwa mtu mwenye furaha ya juu kabisa katika maisha yako?"

Femi akasema:

"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha na hatimaye nikaelewa maana ya furaha ya kweli."

Hatua ya kwanza ilikuwa kukusanya utajiri na nyenzo mbalimbali. Lakini hatua hii haikunipatia furaha niliyoitaka.

Kisha ikaja hatua ya pili ya kujikusanyia vitu vya bei kubwa na vya thamani. Lakini nikagundua kuwa faida yake ni ya muda mfupi na thamani yake haidumu kwa muda mrefu.

Kisha ikaja hatua ya tatu ya kupata miradi mikubwa. Nilikuwa namiliki asilimia 95 ya ugavi wa diesel nchini Nigeria na Afrika. Pia nilikuwa namiliki meli kubwa kabisa Afrika na Asia. Lakini hata hapa sikupata furaha niliyoitazamia.

Hatua ya nne ni pale rafiki yangu mmoja aliponiomba ninunue vitu vya magurudumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu. Idadi yao ilikuwa takribani 200.

Kutokana na ombi hilo la rafiki yangu, nilinunua viti hivyo mara moja.


Lakini rafiki yangu huyo alinisisitiza kwamba niende naye na kuvikabidhi viti hivyo kwa watoto wale. Nilijiandaa na kusuhubiana naye.

Tulipofika kule niliwakabidhi watoto wale kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona mng'ao wa furaha ya ajabu kwenye nyuso za watoto. Niliwaona wote wakiwa wamekalia viti vile wakizunguka na kufurahia.

Ilikuwa kana kwamba wamefika kwenye eneo la michezo na wanafurahia zawadi ya ushindi.

Nilihisi raha ya KWELI moyoni mwangu. Nilipotaka kuondoka, mtoto mmoja aliishikilia miguu yangu. Nilijaribu kuiondosha taratibu lakini alinitazama usoni na kuishikilia zaidi.

Niliinama na kumuuliza: Je, wahitaji kitu kingine?

Jibu la mtoto sio tu lilinipatia furaha bali pia lilibadilisha moja kwa moja mtazamo wangu kuhusu maisha. Mtoto yule aliniambia:

"Nataka kuukumbuka uso wako ili nikikutana na wewe mbinguni, niweze kukutambua na kukushukuru tena."

*Ungependa kukumbukwa kwa lipi baada ya kuondoka ofisini au mahala fulani?

Je, mtu kuhitaji kuukumbuka uso wako tena ni muhimu kwako?

Hili lilinifanya nitafakari. Nakuombea nawe utafakari pia.

Imetafsiriwa na: Kabuga Kanyegeri imesambazwa na Malima Mendy Akili

Akili yenye afya inategemea na malengo makubwa uliyojiwekea na yakafanikiwa kwa kiwango kikubwa, Kinachoturudisha nyuma ...
01/12/2020

Akili yenye afya inategemea na malengo makubwa uliyojiwekea na yakafanikiwa kwa kiwango kikubwa, Kinachoturudisha nyuma ni maamuzi sahihi ndani ya Muda sahihi na akili zetu kudumaa zaidi.

Address

TEMEKE
Dar Es Salaam

Telephone

+255717070823

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AKILI's Mendy Product. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to AKILI's Mendy Product.:

Share