10/06/2023
*𝗡I 𝗨𝗢𝗩𝗨 𝗔𝗖𝗛𝗔*✋
Jambo la kunasibisha ama kutambulisha tabia chafu za baadhi ya Watu kwa makabila yao ni jambo Ovu, Liepuke✋
Mara kadhaa nimesikia watu wakisema👇
👉𝗨𝘀𝗶𝗼𝗲 𝗮𝘂 𝗞𝘂𝗼𝗹𝗲𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗪𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗮 𝗞𝗔𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗹𝗶𝗹𝗲, 𝗻𝗶 𝗠𝗮𝗹𝗮𝘆𝗮 𝘀𝗮𝗻𝗮,
Au
👉𝗨𝘀𝗶𝗼𝗲 𝗮𝘂 𝗞𝘂𝗼𝗹𝗲𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗪𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗮 𝗞𝗔𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗹𝗶𝗹𝗲, 𝗻𝗶 𝗪𝗮𝘀𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗶𝗻𝗮 𝘀𝗮𝗻𝗮,
Au
👉𝗞𝗔𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗹𝗶𝗹𝗲 𝗹𝗶𝗻𝗮𝘀𝗶𝗳𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗧𝗮𝗯𝗶𝗮 𝗖𝗵𝗮𝗳𝘂, 𝘂𝘀𝗶𝗲𝗻𝗱𝗲 𝗸𝘂𝗼𝗮 𝗽𝗮𝗹𝗲 𝗮𝘂 𝗸𝘂𝗼𝗹𝗲𝘄𝗮 𝗻𝗮𝗼.
___
Hayo maneno kutoka kwa vinywa vya watu wasio na hoja wala dalili nimeyasikia sana tu. Ama kwa hakika ni dhana potofu🚮 isiyo na hoja za kiakili wala dalili za Kimaandiko kuchafua Makabila ya wengine kwa Uchafu wa wachache wao.
➡️Hoja ya kusema, Watu wa Kabila fulani ni Malaya, je! Umechunguza kabila zima, maana kabila si kikundi cha watu watano au kumi bali kabila ni mjumuiko watu wengi.
➡️Hoja ya kusema, Kabila lile watu wake wamekithiri kwa Ushirikina, je! Umepata data za kila mtu ndani ya kabila hilo? Au je! umepata Elimu ya ghaibu kufahamu hata yale yaliyofichika kwa Watu?
Kwa kuchafua Makabila ya wengine kwa uchafu ufanywao na wachache wao, huo ni Uovu na ni kujiona kabila lako ni bora kuliko wengine (UKABILA). Na Mtume (صلى الله عليه وسلم) amekemea sana suala zima la Ukabila.
Jubair Ibn Mut'im رضي الله عنه aliarifu: Mtume wa Allah (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙎𝙞 𝙢𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙚𝙩𝙪 𝙮𝙪𝙡𝙚 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙖𝙣𝙖𝙞𝙩𝙞𝙖 𝙐𝙠𝙖𝙗𝙞𝙡𝙖. 𝙎𝙞 𝙢𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙚𝙩𝙪 𝙮𝙪𝙡𝙚 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙖𝙣𝙖𝙥𝙞𝙜𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙖𝙟𝙞𝙡𝙞 𝙮𝙖 𝙐𝙠𝙖𝙗𝙞𝙡𝙖. 𝙎𝙞 𝙢𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙚𝙩𝙪 𝙮𝙪𝙡𝙚 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙠𝙖𝙛𝙖 (𝙞𝙡𝙝𝙖𝙡𝙞) 𝙖𝙠𝙞𝙛𝙪𝙖𝙩𝙖 𝙢𝙬𝙚𝙣𝙚𝙣𝙙𝙤 𝙬𝙖 𝙐𝙠𝙖𝙗𝙞𝙡𝙖."
((𝖲𝗎𝗇𝖺𝗇 𝖠𝖻𝗂 𝖣𝖺𝗐𝗎𝖽, 5121))
((𝖣𝖺𝗋𝖺𝗃𝖺: 𝖧𝖺𝗌𝖺𝗇))
____
𝖬𝗍𝗎 𝗆𝗐𝖾𝗇𝗒𝖾 𝖿𝗂𝗄𝗋𝖺 𝖺𝗎 𝗆𝗍𝖺𝗓𝖺𝗆𝗈 𝗐𝖺 𝖴𝗄𝖺𝖻𝗂𝗅𝖺 𝗇𝗂 𝗄𝖺𝗆𝖺 𝗆𝖿𝖺𝗇𝗈 𝗐𝖺 𝗇𝗀𝖺𝗆𝗂𝖺 𝖺𝗅𝗂𝗒𝖾𝗍𝗎𝗆𝖻𝗎𝗄𝗂𝖺 𝗄𝗂𝗌𝗂𝗆𝖺𝗇𝗂, 𝗄𝗂𝗌𝗁𝖺 𝖺𝗄𝖺𝖿𝖺 𝗇𝖺 𝗄𝗎𝗈𝗓𝖺, 𝗇𝖺 𝗆𝗐𝗂𝗌𝗁𝗈𝗐𝖾 𝗂𝗄𝖺𝗅𝖺𝗓𝗂𝗆𝗂𝗄𝖺 𝗄𝗎𝗏𝗎𝗍𝗐𝖺 𝗇𝗃𝖾 𝗒𝖺 𝗄𝗂𝗌𝗂𝗆𝖺 𝗄𝗐𝖺 𝗄𝗎𝗍𝗎𝗆𝗂𝖺 𝗆𝗄𝗂𝖺 𝗐𝖺𝗄𝖾.
Amesema Mtume wa Allah (صلى الله عليه وسلم)👇
"𝙈𝙛𝙖𝙣𝙤 𝙬𝙖 𝙢𝙩𝙪 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙖𝙣𝙖𝙪𝙣𝙜𝙖 𝙢𝙠𝙤𝙣𝙤 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙬𝙖𝙠𝙚 𝙥𝙖𝙨𝙞 𝙣𝙖 𝙝𝙖𝙠𝙞 (𝙪𝙠𝙬𝙚𝙡𝙞 𝙬𝙖 𝙟𝙖𝙢𝙗𝙤 𝙝𝙪𝙨𝙞𝙠𝙖) 𝙣𝙞 𝙠𝙖𝙢𝙖 𝙢𝙛𝙖𝙣𝙤 𝙬𝙖 𝙣𝙜𝙖𝙢𝙞𝙖 𝙢𝙛𝙪 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙠𝙖𝙩𝙪𝙢𝙗𝙪𝙠𝙞𝙖 𝙠𝙞𝙨𝙞𝙢𝙖𝙣𝙞 𝙣𝙖 𝙖𝙠𝙖𝙫𝙪𝙩𝙬𝙖 (𝙖𝙠𝙖𝙤𝙣𝙙𝙤𝙨𝙝𝙬𝙖) 𝙠𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙩𝙪𝙢𝙞𝙖 𝙢𝙠𝙞𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙚."
((𝘔𝘶𝘴𝘯𝘢𝘥 𝘈𝘩𝘮𝘢𝘥, 3670))
((𝘋𝘢𝘳𝘢𝘫𝘢: 𝘚𝘢𝘩𝘪𝘩))
____
Mtu ambaye ametumbukia kwenye dhambi hii ya Ukabila ameangamia, ndiyo k**a tu ngamia aliyetumbukia kwenye kisima hadi kifo chake kikamfika, kwa hakika Mzoga wake utatia sumu kisima cha mji mzima. Hii ina maana kwamba mwenye Ukabila huchafua taswira ya Kabila zima la wengineo huku akilipa usafi kabila lake. Huyu hana tofauti na mzoga wa ngamia uliofia kisimani na kuoza, na hauna budi kuondoshwa.
Si vyema watu au kikundi cha watu kujiona wao ni bora zaidi na wengine kuwaona waovu zaidi. Vivyo hivyo si vyema kuliona kabila lako ni bora zaidi kitabia huku ukichafua hadhi ya makabila mengineo kwa kuyanasibisha na tabia chafu na mbaya k**a Umalaya au Ushirikina.
Imepokewa kutoka kwa 'Aisha (رضي الله عنها) kwamba, Mtume wa Allah (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙈𝙪𝙤𝙫𝙪 𝙯𝙖𝙞𝙙𝙞 𝙢𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙖 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙣𝙞 𝙢𝙩𝙪 𝙖𝙣𝙖𝙮𝙚𝙢𝙩𝙪𝙨𝙞 𝙢𝙩𝙪 𝙢𝙬𝙚𝙣𝙜𝙞𝙣𝙚 𝙝𝙪𝙠𝙪 𝙖𝙠𝙞𝙙𝙝𝙖𝙡𝙞𝙡𝙞𝙨𝙝𝙖 𝙆𝙖𝙗𝙞𝙡𝙖 𝙯𝙞𝙢𝙖; 𝙣𝙖 𝙢𝙩𝙪 𝙖𝙣𝙖𝙮𝙚𝙢𝙠𝙖𝙣𝙖 𝘽𝙖𝙗𝙖 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙢𝙨𝙝𝙪𝙩𝙪𝙢𝙪 𝙈𝙖𝙢𝙖 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙠𝙬𝙖 𝙐𝙯𝙞𝙣𝙯𝙞."
((𝘚𝘶𝘯𝘢𝘯 𝘐𝘣𝘯 𝘔𝘢𝘫𝘢𝘩, 3761))
((𝘒𝘐𝘵𝘢𝘣𝘶 𝘤𝘩𝘢 33, 𝘏𝘢𝘥𝘪𝘵𝘩 105))
((𝘋𝘢𝘳𝘢𝘫𝘢 𝘏𝘢𝘴𝘢𝘯/𝘋𝘢𝘳𝘶𝘴𝘚𝘢𝘭𝘢𝘢𝘮))
___
Katika Hadith nyingine, Mtume wa Allah (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙈𝙪𝙤𝙫𝙪 𝙯𝙖𝙞𝙙𝙞 𝙢𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙣𝙞 𝙢𝙬𝙖 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙣𝙞 𝙢𝙨𝙝𝙖𝙞𝙧𝙞 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙮𝙚 𝙝𝙪𝙙𝙝𝙖𝙡𝙞𝙡𝙞𝙨𝙝𝙖 𝙠𝙖𝙗𝙞𝙡𝙖 𝙯𝙞𝙢𝙖."
((𝘈𝘭-𝘈𝘥𝘢𝘣 𝘢𝘭-𝘔𝘶𝘧𝘳𝘢𝘥, 870))
((𝘋𝘢𝘳𝘢𝘫𝘢: 𝘚𝘢𝘩𝘪𝘩))
____
Kwa mujibu wa hadithi hizo za Mtume صلى الله عليه وسلم, haifai Mtu kulichafua ama kulidhalilisha Kabila zima kwa Uchafu wa wachache miongoni mwao. Uislamu unakataza kujumuisha makosa ya wachache kwa jopo la walio wengine, yaani hairuhusiwi kuchafua kundi zima la watu kwa uchafu wa wachache wao. Kwa sababu watu wasio na hatia hawawezi kuwajibishwa kwa makosa ya wengineo. ALLAH TAALAH amesema ndani ya Qur'an👇
ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ
(AL - AN-A'AM - 164)
"..Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana."
____
Na katika Hadithi iliyopokelewa na Abdullah Ibn Mas'ud aliarifu: Mtume wa Allah (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙈𝙩𝙪 𝙖𝙨𝙞𝙖𝙙𝙝𝙞𝙗𝙞𝙬𝙚 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙠𝙤𝙨𝙖 𝙮𝙖 𝘽𝙖𝙗𝙖 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙖𝙪 𝙣𝙙𝙪𝙜𝙪 𝙮𝙖𝙠𝙚."
((𝘚𝘶𝘯𝘢𝘯 𝘈𝘯-𝘯𝘢𝘴𝘢𝘪, 4131))
((𝘋𝘢𝘳𝘢𝘫𝘢: 𝘚𝘢𝘩𝘪𝘩))
Hapa tunajifunza kuwa si vyema kumuingiza mtu makosani kwa kosa alilolifanya mwengine eti kwa sababu tu ya Unasaba. Na vivyo hivyo, haifai kuliingiza kabila zima makosani kwa makosa yafanywayo na wachache ndani yake, watiwe makosani wao k**a wao.
______
𝗨𝗞𝗔𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗡𝗔 𝗡𝗗𝗢𝗔
Hakuna Aya yoyote ile ndani ya Qur'an, wala hakuna Hadithi Sahih au dhaifu ambazo zimetaja kwamba, moja kati ya kigezo cha kuoa au kuolewa ni kutazama Kabila la mtu. Aya hiyo au hadithi hiyo hakuna. Bali vigezo alivyovitaja Mtume (صلى الله عليه وسلم) ni k**a vilivyoelezwa katika Hadithi zifauatazo👇
Abu Hurayrah (رضي الله عنه) ameeleza kuwa: Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙈𝙬𝙖𝙣𝙖𝙢𝙠𝙚 𝙖𝙣𝙖𝙤𝙡𝙚𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙫𝙞𝙩𝙪 𝙫𝙞𝙣𝙣𝙚: 𝙠𝙬𝙖 𝙪𝙩𝙖𝙟𝙞𝙧𝙞 𝙬𝙖𝙠𝙚, 𝙠𝙬𝙖 𝙪𝙟𝙪𝙯𝙞 𝙬𝙖𝙠𝙚, 𝙠𝙬𝙖 𝙪𝙯𝙪𝙧𝙞 𝙬𝙖𝙠𝙚 𝙣𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙙𝙞𝙣𝙞 𝙮𝙖𝙠𝙚. 𝙈𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙚 𝙮𝙪𝙡𝙚 𝙢𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙢𝙨𝙞𝙢𝙖𝙢𝙤 𝙢𝙯𝙪𝙧𝙞 𝙬𝙖 𝘿𝙞𝙣𝙞."
((𝘉𝘶𝘬𝘩𝘢𝘳𝘪 𝘯𝘢 𝘔𝘶𝘴𝘭𝘪𝘮))
Kigezo kikuu ambacho Mtume (صلى الله عليه وسلم) amekipendekeza kwa Mwanamke kuolewa ni Msimamo mzuri wa Dini yake.
Katika hadithi nyingine, Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema👇
"𝙋𝙞𝙣𝙙𝙞 𝙖𝙣𝙖𝙥𝙤𝙠𝙪𝙟𝙞𝙚𝙣𝙞 𝙢𝙣𝙖𝙚𝙧𝙞𝙙𝙝𝙞𝙖 𝘿𝙞𝙣𝙞 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙣𝙖 𝙩𝙖𝙗𝙞𝙖 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙣𝙞 𝙣𝙯𝙪𝙧𝙞, 𝙗𝙖𝙨𝙞 𝙢𝙪𝙤𝙯𝙚𝙨𝙝𝙚𝙣𝙞..𝙆𝙖𝙢𝙖 𝙝𝙪𝙩𝙖𝙛𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙝𝙞𝙫𝙮𝙤 𝙥𝙖𝙩𝙖𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙣𝙖 𝙝𝙪𝙯𝙪𝙣𝙞 (𝙢𝙖𝙩𝙖𝙩𝙞𝙯𝙤) 𝙣𝙖 𝙫𝙪𝙧𝙪𝙜𝙪 𝙠𝙖𝙩𝙞𝙠𝙖 𝙪𝙡𝙞𝙢𝙬𝙚𝙣𝙜𝙪."
___
Kwa hiyo hapa tunaona sifa za Mume zilizotajwa ni mbili tu, Dini na tabia yake njema. Hapo hakuna Sifa ya UKABILA ili Kuonesha kwamba Ukabila hauna nafasi katika UISLAMU.
Si Mbora wala Mwema kwa Ukabila au Utaifa wake, bali Mbora mbele ya ALLAH ni yule mwenye Kumcha Yeye tu👇
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ
(AL H'UJURAAT - 13)
"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu (mbora) zaidi kati yenu kwa Allah ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Allah ni Mwenye kujua, Mwenye khabari."
___
Hakuna mbora kwa Kabila wala Taifa lake, bali aliye mbora ni yule mwenye Kumcha ALLAH TAALAH zaidi katika Waja wake.
___
HIVYO BASI, FIKRA AU MTAZAMO HASI AU CHANYA WA UKABILA HAUNA NAFASI KATIKA UISLAMU.
Tabia ya Umalaya, Ushirikina na kadhalika, Si alama au Nembo ya Kabila fulani, bali Tabia hizo ni matamanio ya wahusika wenyewe. Hata huyo anayekashifu Makabila ya watu kwa Umalaya, usikute na yeye pia ana machafu yake makubwa tu likiwemo na hilo pia.
____
𝙒𝘼𝙇𝙇𝘼𝙃𝙐 𝘼'𝙇𝘼𝙈
𝙉𝘼𝙈𝙐𝙊𝙈𝘽𝘼 𝘼𝙇𝙇𝘼𝙃 𝘼𝙏𝙐𝙊𝙉𝙂𝙊𝙕𝙀 𝙆𝘼𝙏𝙄𝙆𝘼 𝙐𝙏𝙄𝙄𝙁𝙐 𝙒𝘼𝙆𝙀, 𝘼𝙈𝙄𝙄𝙉
__________