Catholic_OG

Catholic_OG

02/06/2024

Heri ya sikukuu ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo mkombozi wa dunia

Mtu yeyote anayelipinga Kanisa Katoliki asitumie Biblia, atumie kitu kingine; kwasababu Biblia ni kitabu cha Kanisa kato...
04/02/2024

Mtu yeyote anayelipinga Kanisa Katoliki asitumie Biblia, atumie kitu kingine; kwasababu Biblia ni kitabu cha Kanisa katoliki. Historia inadhibitisha hilo kwa sababu Yesu alikuwa haongei na kuandika na wala hakuwa na Katibu na wala hakuacha maagizo ya kuandika Biblia🇻🇦

MAMBO 10 KILA MKRISTO AFAHAMU.
1. Hakukuwa na Biblia kwa miaka 399 BK ya kwanza baada ya Kristo ( Kanisa Katoliki ndilo lililo anza na baadaye ndiyo ikaandikwa Biblia )

2. Kanisa katoliki ndilo lililoamua kuwa na biblia kwa kuchagua vitabu 27 kati ya vitabu zaidi ya 300 vya Injili, nyaraka na kuviita Agano Jipya.

3. Padre Tertullian ndiye alitoa jina la "Agano Jipya" kwa Biblia Takatifu, pia ndiye mwandishi wa Kilatini mzee zaidi.

4. Ni kanisa katoliki ndilo lililoamua ni vitabu vipi viingizwe katika Agano Jipya baada ya kusambaa hati nyingi za uongo.

5. Ni kanisa katoliki ndilo lililotoa Biblia kwa Ulimwengu kwa ajili ya kuwarahisishia waumini wao wakatoliki kujisomea k**a kitabu kimoja chenye vitabu vingi ( Hakukuwa na madhehebu yoyote ya kiprotestant mpaka mwaka 1517 )

6. Mwaka 367 baada ya Kristo, mtakatifu Papa Damasius wa kwanza akiwa na baraza wakati wa upapa wake alichagua hati za maandiko ambazo aliona ni za kweli zilizovuviwa na Roho mtakatifu.

7. Tamko la baraza la Roma chini ya papa Damascus wa kwanza mwaka 382 BK ndiyo lilio halalisha Biblia takatifu.

8. Vitabu rasmi 27 viliongezwa kwenye hati au vitabu 46 vya Agano la Kale na kusababisha mkusanyiko mmoja wa vitabu 73 uitwao Biblia.

9. Mwaka 367 hadi 397 BK mtakatifu Padre Jerome akisaidiwa na Roho Mtakatifu alitafsiri maandiko katika wa miaka 30 na kuiita Biblia Jerusalem. yeye ni padre Mkatoliki, mwanatheolojia na daktari wa kanisa, alizungumza Kigiriki, Kiebrania na Kilatini; Pia alisoma Kiaramu Lugha ya Yesu alivyozungumza.

10. Papa Mtakatifu Siricius ndiye aliyeyaita Maandiko Matakatifu BIBLIA maana yake ni mkusanyo wa vitabu. Na Askofu Mkuu Steven Langton na Kardinali Hugo Desancto Caro wanasifiwa kwa kuunda Sura na mistari au aya katika Biblia yote.

NB
Martin Luther mwanzilishi wa kwanza wa madhehebu kutoka kanisa Katoliki alisema "Tunawashukuru Kanisa Katoliki, Bila Kanisa Katoliki tusingekuwa na Biblia Takatifu" mwaka 1517 ujerumani.

K**a unajivunia kuwa mkatoliki weka "Aminaaaa"

Play ⏯️ My Music now Enjoy Favorite Music EverdayLike my Pages Click here 👇
06/01/2024

Play ⏯️ My Music now Enjoy Favorite Music Everday
Like my Pages
Click here 👇

Learn more about ♫ Dona Jr ♫ online from ❱ Mdundo.com ❰ Stream and download high quality mp3 and listen to popular playlists.

NJOONI NANYI MTAONA.*Yoh.1:36-39.* *Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!* Wale wanafunzi ....
04/01/2024

NJOONI NANYI MTAONA.

*Yoh.1:36-39.*

*Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!*
Wale wanafunzi .. wakamfuata Yesu. .. Mnatafuta nini?
Akawaambia, *Njooni, nanyi mtaona.* Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
Umeenda kwake mara ngapi!
Ukitembea wanakusemaje!
Unatembeaje ili wakutambue?
Kwako ni wapi!
Umewapeleka kwa Yesu wangapi!
Umekaa kwake muda wa saa ngapi?

*Anatualika na kutukaribisha, njoni nanyi mtaona.*

09/12/2023

08/12/2023

*Wanaume hoyeee...!!! Hatimaye tumepata wimbo maalum.*

27/11/2023

Reposted from  “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”Mithali 28:13Tena“T...
07/11/2023

Reposted from “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

Mithali 28:13

Tena

“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”

1 Yohana 1:9

Baba Mtakati Francisko amemteua Padre  Eusebio Samwel Kyando kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Njombe Tanzania. Alizaliwa...
19/10/2023

Baba Mtakati Francisko amemteua Padre Eusebio Samwel Kyando kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Njombe Tanzania. Alizaliwa tarehe 7 Machi 1964 huko Njombe. Baada ya majiudo yake ya Seminari ndogo ya Mtakatifu Kizito Mafinga, Jimbo la Iringa, aliendelea na falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustine Peramiho.Songea

Na alipewa darala la upadre mnamo tarehe 19 Juni 1996

14/08/2023

*MAFUNDISHO(DOGMA)YA KANISA KATOLIKI KUHUSU BIKIRA MARIA*

Na *Padre Titus Amigu*

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu:
*1. Bikira* *Maria* mkingiwa dhambi ya asili
*2. Bikira* *Maria* Mama wa Mungu
*3. Bikira* *Maria* Bikira daima
*4. Bikira* *Maria* kupalizwa mbinguni mwili na roho

*MKINGIWA DHAMBI YA ASILI*
Malaika alimsalimia Maria *“umejaa neema”* (Lk 1:28) maana ndiye tunda bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi dhambi ya asili na madonda yanayotokana nayo, wala asitende dhambi maisha yake yote. Kwa maneno mengine, Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna bora kushinda viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita “A Panagia” = “Mtakatifu tu”. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira Maria alijitambulisha k**a Mkingiwa kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi (Ufaransa). Tena mwaka 1917 huko Fatima (Ureno) aliwafunulia Lusia, Fransisko na Yasinta Marto moyo wake safi usio na doa.

*MAMA WA MUNGU*
Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu k**a sisi katika yote isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu: akisema, ‘Mimi’, ni kwa Nafsi yake hiyo. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, *“Kweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo”* (Yoh 8:50). “K**a vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, *“Wakati maalumu ulipotimia Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke”* (Gal 4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika. *“Malaika alimwambia, ‘Hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’”* (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa Efeso uliomuita *“Mzazi wa Mungu”,* ukisema Maria anastahili kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: *“Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.* Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” (Lk 1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti likakamilishwa na Mtume Thoma aliyemuambia Yesu mfufuka: “ *Bwana wangu na Mungu wangu!”* (Yoh 20:28)

*BIKIRA NA MAMA*
Wakristo na Waislamu wote wanakiri kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango wa mwanamume. La ajabu zaidi katika imani hiyo ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili inasita, ni lazima kukiri na malaika, *“Hakuna lisilowezekana kwa Mungu”* (Lk 1:38). Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa.

Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa “ *Bikira daima”* kwa sababu alimchukua mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa inajitokeza katika jibu alilompa malaika aliyemtabiria mimba: “Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Lk 1:35). Ni kielelezo cha Wakristo ambao Mtume Paulo aliwaandikia: “Nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2Kor 11:2), “mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine” (1Kor 7:35).
*Wanaosemwa katika Injili “ndugu zake Yesu” si watoto wa Bikira Maria, bali ndugu wa* *ukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu.* K**a Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, Yesu angekuwa amefanya kosa la kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, *“‘Mwana, tazama Mama yako’. Na tangu saa ile huyo* *mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake”* (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo “ndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na mama yao kwenye Injili anaitwa *“Maria mwingine”,* si Maria Mama wa Yesu. *“Walikuwepo pia wanawake waliotazama kwa mbali. Miongoni* *mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na* *Maria mama wa akina Yakobo mdogo na Yose”* (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue kuwatofautisha kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira Maria k**a *“Mama wa Yesu”.*

*KUPALIZWA MBINGUNI MWILI NA ROHO*
Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya mwanamke mshindi. “Ishara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio lake yametimia: Mungu *“amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza”*(Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale, yanavyoshuhudiwa na Mababu wa Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius XII kwa niaba ya maaskofu wote mwaka 1950.
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba *Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu*
Hapo zamani hakuna mkristu au dhehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia K**a ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu K**a tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “ *Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.”* 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, *“Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.* 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, *“Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?”* 35 Malaika akamjibu, *“Roho Mtakatifu atakushukia,* na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia k**a kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, *“Amka!* Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: *“Ataitwa Mnazare.”* Matayo 2:19-23
K**a wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima k**a familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo k**a ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, *“Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.”* 49 Yeye akawajibu, *“Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?”* 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. K**a wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao k**a Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.
4. Kukosekana kwa neno *“Binamu”* kwenye lugha ya Yesu
Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno *“Binamu”* kwa hiyo mabinamu walijulikana k**a dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno k**a; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa k**a kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu *(Dada na Kaka)* wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
*KISWAHILI* 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
*ENGLISH* 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, *“Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.”* (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. *(Matayo 27:55-56)*
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. *(Wagalatia 1:19)*
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. *(Yuda 1:1)*
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. *(Yohana 19:25)*
Kwa hiyo kwenye *(Yohana 19:25)* tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye *(Matayo 27:55-56)* wametajwa ni Mama za kina nani k**a inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)

Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: *“Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.”* Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.
Endelea Na Hizi:
Nafasi ya Bikira Maria Katika Kanisa Katoliki Kanisa katoliki linamthamini Bikira Maria k**a Mama wa Mungu, Mama wa Kristu, Mama wa Mkombozi pia Mama wa uhai kuna...
Mafundisho Kuhusu Bikira Maria

*DOGMA ZA KANISA KATOLIKI KUHUSU BIKIRA MARIA.*
Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana naufunuo...

*MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA*
Leo nimeamua kutoa makala kuhusu Bikira Maria Baada ya maswali mbalimbali kuibuka kuhusu nafasi yake kwetu sisi. Chanzo cha makala...
Mafundisho na mapokeo Katika Kanisa Katoliki yanapopatikana kwenye Biblia Wakatoliki wengi huyumbishwa kwa kuambiwa huamini mambo ambayo hayako au ni kinyume na Biblia. Aya zifuatazo zitakusaidia wewe mkatoliki kuelewa...
Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine? Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. VilevileMt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume...
Heshima za Liturujia kwa Bikira Maria Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia ya Kiroma. Hapa zimepangwa kulingana na heshima zinavyozidiana: Sherehe8 Desemba –...
Maana ya jina Bikira Maria Jina asili kwa Kiaramu ni מרים, Maryām lenye maana ya “Bibi”; watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania wanaojulikana k**a...
Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili...

*MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI MITAGUSO MIKUU*

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro....
Biblia inavyothibitisha kuwa Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote (Ufunuo 12:17-17) Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa...

*JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?*

Wakatoliki wengi huyumbishwa kwa kuambiwa huamini mambo ambayo hayako au ni kinyume na Biblia. Aya zifuatazo zitakusaidia wewe mkatoliki kuelewa...
Jinsi Bikira Maria anavyoelezwa Katika dini ya Kiislamu Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na...
Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye Kwa hiyo Mitume na wakristu wa mwanzoni hawakuwa kumuomba wakati akiwa hai. Ila Baada ya Kifo chake na kupalizwa kwake...
Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho

*Tumsifu Yesu Kristo!*

Na *FR. TITUS AMIGU*

*NDOA ZA MSETO NI NINI, NA ZINAFANYIKAJE KATIKA KANISA KATOLIKI?*Katika Kanisa Katoliki, ndoa kati ya Mkatoliki na asiye...
28/07/2023

*NDOA ZA MSETO NI NINI, NA ZINAFANYIKAJE KATIKA KANISA KATOLIKI?*

Katika Kanisa Katoliki, ndoa kati ya Mkatoliki na asiye Mkatoliki inajulikana k**a "ndoa ya mseto." Ingawa maelezo mahususi yanaweza kutofautiana kidogo kulingana na mahalia pamoja na hali zinazohusika, kuna miongozo ya jumla inayofuatwa na Kanisa katika kesi k**a hizo.

1. RUHUSA KUTOKA KWA ASKOFU MAHALIA
Mkristo Mkatoliki (katika kesi hii, bibi harusi) lazima apate kibali kutoka kwa askofu wa jimbo ili kuolewa na mtu ambaye si Mkatoliki. Ruhusa hii inajulikana k**a "mwongozo kutoka kwa tofauti ya ibada" na inatolewa ikiwa masharti fulani yatatimizwa (Kan. 1125)

2. UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA NDOA
Upande wa Mkristo mkatoliki anatakiwa kushiriki katika uchunguzi kabla ya ndoa ili kuhakikisha kwamba yuko huru kuolewa na kwamba wanaelewa wajibu na wajibu wa ndoa ya Kikatoliki.

3. UHURU WA KUTENDA IMANI
Upande wa mtu asiye Mkristo Mkatoliki kisicho cha lazima afahamishwe kwamba Mkristo Mkatoliki yuko huru kutekeleza imani yake na kutimiza wajibu wake wa kidini. Mshirika asiye Mkatoliki anatarajiwa kuheshimu na kuunga mkono imani ya Mkatoliki na, ikiwezekana, kukubali kulea watoto wote katika imani ya Kikatoliki.

4. KUJIANDAA KWA NDOA Wanandoa wanatakiwa kushiriki katika mafundisho ya maandalizi ya ndoa au kuhudhuria ushauri kabla ya ndoa. Hii ni kuwasaidia kuelewa sakramenti ya ndoa, umuhimu wake, na changamoto wanazoweza kukabiliana nazo k**a wanandoa.

5. RUHUSA YA KUOA KATIKA SHEREHE ISIYO YA KIKATOLIKI Katika baadhi ya matukio, askofu anaweza kutoa kibali cha ndoa mseto kufanyika katika sherehe isiyo ya Kikatoliki ikiwa chama kisicho cha Kikatoliki kinafuata mila tofauti ya kidini na ni muhimu. ili wawe na sherehe zao za kidini.

Ni muhimu kutambua kwamba wakati Kanisa Katoliki linaruhusu ndoa mseto na linahimiza Mkristo Mkatoliki kuoa ndani ya imani ya Kikatoliki wakati wowote iwezekanavyo. Hii ni kuhakikisha msingi imara katika imani na maadili ya pamoja, ambayo yanaweza kuchangia ustawi wa wanandoa na watoto wowote wa baadaye.

Inaendelea kwenye comments

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Catholic_OG posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share