14/02/2025
UNAZIFAHAMU BALO ZA MTUMBA KUTOKA KOREA?
Wauza balo wengi wanapokupa Bei za balo,balo zinazotoka Korea huwa zinakuwa juu kidogo ukilinganisha na zinazotoka China.na sisi tunaamini hili la Bei kubwa litakuwa zuri kuliko la Bei ndogo.kwakuwa unahitaji ukute mzigo mzuri,unajitoa kuchukua la Korea kwa Bei kubwa.ukifungua unapata presha.
Kwanza unauhakika Ni la Korea? Zipo kampuni nyingi za mabalo kutoka Korea,Zina nembo tofauti tofauti zenye rangi tofauti tofauti.hizo nembo ndo unapaswa kuzifahamu na ukichagua balo unachagua nembo unayohitaji.mfano nembo ya BEA.hii imeandikwa BEA na inaalama ya kidole gumba.ni Kati ya balo zenye nguo nzuri,ila Ina grade.
Kila rangi ya nembo ya Bea inamaana yake,na kila namba ya kwenye nembo Ina maana yake.mfano BEA 78 Ni balo la gauni.ila hiyo 78 pink,Ni gauni za Aina zote,zimechanganywa na Ni grade A.
BEA 78 ya njano Ni gauni ndefu grade A.kwahiyo unatakiwa kuzifahamu vyema ili usiombe tu naomba balo la Korea,unapewa grade 3 unaanza kulalamika.