05/11/2025
Anaandika πππ
Yeyote aliyehusika na machafuko haya kwa namna yoyote lazima awajibike, iwe kwa kuchochea mitandaoni au kwa kutenda moja kwa moja, basi hatua kali zichukuliwe. Tunayo nchi moja tu na uhai ni mmoja tu.
Haki ya kila mmoja ipatikane! Poleni sana ndugu zetu mliofikwa na majanga kwa kuharibiwa mali za umma na mali za watu binafsi ama kujeruhiwa ama maafa zaidi!
Ili tuyatazame mambo haya kwa wigo mpana na kwa akili huru, tusijifungie katika eneo moja tu box la demokrasia na haki tu, lazima tujifunze kutazama nyuma ya pazia.
Tuwatazame wakubwa duniani Magharibi na Mashariki, Ni wazi wakubwa hawa wako kwenye vita vya uchumi, siku za nyuma usharika wa Dar na Moscow ulipokomaa niliwahi kutahadharisha nikihoji je tuko tayari k**a taifa kucheza Disco la Washington na Brussels? Nilikuwa nikisema hayo nikifahamu wazi kwamba mataifa mengi yaliyoshibisha usharika na Moscow, tawala zao zimetingishwa na nyingine kudondoshwa kabisa.
Je tunatumika k**a uwanja wa vita vya Uranium na vita vya raslimali zingine adhimu duniani dhidi ya wakubwa? Tuamke tukatae kwa nguvu zote
Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza, Je tulijiandaa vya kutosha kukabila uchochezi wa Ulaya na Marekani tulipoamua kuingia mikataba muhimu ya nyuklia na Urusi? Tulijiandaa kikamilifu kukabili mikikimikiki ya Marekani na Ulaya pale tulipoamua kuongeza ushirika wetu na Moscow baada ya mageuzi ya Sera za Kigeni za Urusi hapo 2023. Leo Urusi na Uchina walikuwepo k**a mashuhuda wa Kiapo cha Rais wa Tanzania. Unafikiri kwa nini Marekani na Nduguze hawakuhudhuria? Sikufundishi kufikiri
Pamoja na matatizo mengi ya utawala wa kiimla wa ccm na serikali yake, pamoja na ukosefu wa haki na demokrasia nchini, Lakini, Hiki ndio kiini cha yote hayo, chini ya mgongo wa demokrasia na haki nchini ambavyo ni kweli na haki na wazi kabisa kwamba serikali ilipuuza maonyo ya haki na demokrasia nchini. Mali na utajiri wa Tanzania vinatungiza kwenye machafuko kwa vita ya Marekani na Urusi
Nini kifan