31/10/2026
Happy Birthday to my lovely son! ❤️👑🎂
Mwanangu, wewe ni moja ya zawadi kubwa na nzuri ambazo Mungu amenipa. Sina maneno ya kuelezea furaha ya kuwa mama yako. Nakupenda kuliko unavyoweza kufikiria, na kila siku namshukuru Mungu kwa ajili yako.
Ombi langu ni Mungu akupe maisha marefu, afya njema, hekima na mafanikio. Akulinde kila unapokwenda na akuongoze katika kila hatua ya maisha yako.
Ninajivunia kuwa mama yako, mwanangu. Wewe ni furaha ya moyo wangu. Nakupenda sana, leo umetimiza miaka 12 hii furaha kubwa mno kwangu
More blessings dear son
Baraka zote za mzaliwa wa kwanza ziwe juu yako
Nakuombea sana