23/11/2019
Daktari Mkuu wa Kitengo cha Ultra Sound katika Hospitali ya Chakechake, Zanzibar Masoud Abdallah mwenye umri wa miaka 53 amekamatwa na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mgonjwa mwenye mimba ili ampatie huduma ya uchunguzi kwa kina.
-
"Huyo Mama Mjamzito alishafika Hospitalini hapo mara tatu mfululizo lakini hakupata matibabu kutokana na Daktari kudai rushwa ya ngono ndipo amuhudumie"-ZAECA
_
Baada ya kuweka mtego tulifanikiwa kumkamata akiwa chooni pamoja na mteja wake na tuliwakuta wakiwa wamevua nguo, tumemuhoji na kumpa dhamana kwakuwa ni haki yake”-ZAECA