WATU WA MUNGU

WATU WA MUNGU 株式会社ewfvds、個人情報保護の重要性に鑑み、「個人情報の保護に関する?

個人情報の定義
お客さま個人に関する情報(以下「個人情報」といいます)であって、お客さまのお名前、住所、電話番号など当該お客さま個人を識別することができる情報をさします。他の情報と組み合わせて照合することにより個人を識別することができる情報も含まれます。
1.個人情報の取得について
当ショップは、偽りその他不正の手段によらず適正に個人情報を取得致します。

2.個人情報の利用について
当ショップは、個人情報を以下の利用目的の達成に必要な範囲内で、利用致します。

以下に定めのない目的で個人情報を利用する場合、あらかじめご本人の同意を得た上で行ないます。

(1) 各種商品・サービスに関する情報やサービス提供及び商品発送に関わる業務のため

(2) 当ショップサービス利用の統計資料作成のため

3.個人情報の安全管理について
当ショップは、取り扱う個人情報の漏洩、滅失またはき損の防止その他の

個人情報の安全管理のために必要かつ適切な措置を講じます。

4.個人情報の委託について
当ショップは、個人情報の取り扱いの全部または一部を第三者に委託する場合は、当該第三者について厳正な調査を行い、取り扱いを委託された個人情報の安全管理が図られるよう当該第三者に対する必要かつ適切な監督を行います。

5.個人情報の第三者提供について
当ショップは、個人情報保護法等の法令に定めのある場合を除き、個人情報をあらかじめご本人の同意を得ることなく、第三者に提供致しません。

6.個人情報の開示・訂正等について
当ショップは、ご本人から自己の個人情報についての開示の請求がある場合、速やかに開示を致します。

その際、ご本人であることが確認できない場合には、開示に応じません。

個人情報の内容に誤りがあり、ご本人から訂正・追加・削除の請求がある場合、調査の上、速やかにこれらの請求に対応致します。

その際、ご本人であることが確認できない場合には、これらの請求に応じません。

05/09/2021
08/07/2021

BWANA YESU ASIFIWE

07/04/2021

JE KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UCHUMBA KABLA YA NDOA NI UPENDO?

Date: December 19, 2020Author: Peter Ogast1
Shalom Vijana wa k**e na wa kiume waTanzania
Nipende
kumshukuru Mungu kwa siku nyingine aliyonipa heshima ili nikuletee somo hili na nina imani kubwa litakusaidia wewe au rafiki yako ama ndugu yako na kukuvusha au kumvusha toka sehemu moja kwenda nyingine zaidi.
Zaburi 119:9 inasema *”Jinsi gani aisafishe njia yake? Kwa kutii,akilifuata neno lako”.*
1Yohana 2:14b-17 *inasema”Nimewaambia ninyi,vijana ,kwasababu mna nguvu,na neno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi mmemshinda yule mwovu.Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia.Mtu akiipenda dunia,kumpenda Baba hakumo ndani yake.Maana kila kilichomo duniani,yaani,tamaa ya mwili,na tamaa ya macho havitokani na Baba,Bali vyatokana na dunia.Dunia inapita,pamoja na tamaa zake, Bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”*
I Wakorintho 3:16 inasema *”Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu,na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.K**a mtu akiliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu mtu huyo.kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu ,ambalo ndilo ninyi*
1 Wakorintho 6:8-9 *inasema”Lakini nawaambia wale wasiooa bado,na wajane,ni heri wakae k**a mimi nilivyo.Lakini ikiwa hawawezi kujizuia,na waoe;maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa*
✔Ndugu zanguni vijana wenzangu wakitanzania kumekuwepo na Changamoto kubwa sana kwa vijana wakatu wakiwa kwenye urafiki au uchumba kuambiana k**a nisipolala na wewe au kufanya na wewe mapenzi haunipendi na wengi wameingia kwenye mtego huo na kuanguka katika uasherati.Kufanya tendo la ndoa si kipimo cha Upendo katika uchumba Bali ni kipimo cha uasherati wenu na uchafu wenu.Ndugu ukisema unampenda mtu hutafanya naye mapenzi maana kwa kufanya hivyo unamkosesha na Mungu wake k**a unampenda mvumilie mpaka siku rasmi ya kufunga ndoa,hivyo mtu yeyote anayedai
anakupenda na huku Upendo wake anataka akutenge na Mungu,mtu huyo ni wakuogopa zaidi ya shetani.Vijana hiyo ni Dhambi na si Upendo hata kidogo,Ikimbieni zinaa na uasherati.
✔ Mwanamume na mwanamke wanapooana, wao
huwa “mwili mmoja.” Watu wawili ambao
hawajaoana wanapofanya Tendo la Ndoa, ambalo huitwa uasherati, wao pia huwa “mwili mmoja,” lakini
huo ni mwili ambao kwa Mungu ni najisi.
Isitoshe, miungano k**a hiyo si upendo Sababu moja ni kwamba uasherati ni ngono bila kuwajibika. Na licha ya kumfanya mtu asijiheshimu, uasherati unaweza kusababisha
magonjwa, mimba isiyotakiwa, na maumivu ya
kihisia. Zaidi ya yote, kufanya hivyo huvunja viwango vya uadilifu kwa Mungu.
Hivyo,uasherati
unaonyesha kwamba mtu hajali sana au hajali
kabisa hali njema na furaha ya sasa na ya wakati ujao ya mtu yule mwingine.
Kwa Mkristo, kufanya uasherati ni kuingilia haki
za ndugu,Kaka au dada yake wa kiroho,Binti ambaye hujamuoa au kijana wa kiume ambaye hujaolewa naye kufanya naye tendo la ndoa ni kufanya na Dada yako au kaka yako uasherati.
Mungu ‘atalipiza adhabu’ kwa ajili ya matendo yote ya uasherati yanayofanywa na watu wasiotubu na kuacha.
✔ una mchumba na mnapanga kuoana. Basi
kwa nini msitumie uchumba wenu kujenga msingi
imara unaotegemea kuaminiana na
kuheshimiana ila mnatumia kudanganya kuwa usipofanya na mimi mapenzi haunipendi nani kakwambia kufanya uasherati ndio Upendo ,huo sio Upendo hiyo tamaa ya mwili na dhambi.Je Mwanamke anawezaje
kumwamini mwanamume ambaye ameonyesha
kwamba hawezi kujizuia kwa tamaa zake? Na je, ni rahisi kwa mwanamume kuthamini na kuheshimu
mwanamke ambaye hupuuza sheria ya Mungu ili
kutosheleza hisia zake za kimwili. Biblia inasema
“yeye aliye na mazoea ya kufanya uasherati
anautendea dhambi mwili wake
mwenyewe.”
✔Kwa wale waliooa inawezekana
Wewe na mke wako mlifanya uasherati kabla ya ndoa na baada ya kuoa ukaona amekuwa mke wako hukuwahi kutubu na unaona mko sahihi tubu juu ya uasherati mliofanya kabla ya kuoana maana mlitenda dhambi, Zidini sana kurudisha uhusiano
mzuri pamoja na Mungu, na kuimarisha uaminifu
kati yenu.
*✔Sina mazuri ya kukuambia kuhusu kufanya mapenzi na mchumba wako ama rafiki yako na kudanganyana kuwa ni Upendo,huo sio Upendo Bali ni kuangamizana,na Kumkosea Jehova aliyeumba hivyo tubu leo na kuacha dhambi hiyo ya uasherati*
🔴 Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua
njema ya kumpokea BWANA YESU ili awe BWANA na MWOKOZI wako
tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu
K**A UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KWA IMANI
”BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi ya uasherati nikidhani ni Upendo kwa mchumba wangu , lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki.
futa jina langu katika kitabu cha hukumu na
uliandike jina langu katika kitabu cha uzima.Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9
na wa 10 Neno lako linasema ”Kwa sababu,
ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni
BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa
MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa
maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,
na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu ” .
BWANA YESU mimi nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika
nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa
dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo
mema na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako
Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na
anasa zote za dunia hii. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani
inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU.BWANA
YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa.kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa
ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika jina la YESU
KRISTO nimeomba na kupokea Amen.”
K**a umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa.

06/04/2021

DALILI ZA SIKU ZA MWISHO (Mathayo 24:3-44)
Nyakati za biblia wanafunzi wa Yesu walimjia Yesu kwa shauku kubwa na kutaka awaambie dalili za kuja kwake na nini dalili za mwisho wa dunia ,Yesu kristo akajibu haya ambayo leo tunayajadili na Yesu pia akaeleza dalili zifuatazo.
a) WATATOKEA WATU WAKISEMA MIMI NI KRISTO (Mathayo 24:5)
Wajiitao kristo wametokea wengi mno duniani na wamedanganya wengi na watu wengi wameangamizwa na hao wajiitao kristo .Hiyo ni dalili miongoni mwa dalili ambazo Yesu amezisema.Yesu akaendelea na kusema,
b) TAARIFA ZA VITA,NJAA ZA KUTISHA NA MATETEMEKO YA NCHI (Mathayo 24:6-8)
Yesu anatupa taarifa kuhusu vita vitakavyotokea duniani na njaa isiyoelezeka katika dunia.Ni kweli njaa duniani zimetokea kwa namna za kutisha kwa mfano ;Ethiopia.Somalia,Tanzania(1978)n.k.Matetemeko ya nchi yametokea duniani hata ikafikia watu wakafa malaki kwa malaki mfano; tetemeko la Haiti,tetemeko k**a Tsunami (tetemeko la chini ya bahari) na matetemeko ya kila namna duniani yametokea ,hayo yote Yesu kristo alikwisha sema.Kuhusu vita vitakuwa katika namna mbalimbali
(a)Taifa kwa taifa . (b) na Ufalme kwa ufalme.
(a) Neno taifa katika maandiko halimaanishi ni nchi,bali linamaanisha kabila lililopo katika nchi moja(Mwanzo 25::22-23) kwa hiyo Taifa kupigana kwa taifa inamaanisha kabila moja kupigana na kabila jingine ndani ya nchi moja, kifupi ni vita vya makabila.
(b) Ufalme kupigana na Ufalme.Neno ufalme katika maandiko linamaanisha nchi.kifupi ufalme kupigana na ufalme ni nchi kupigana na nchi nyingine .Na Hayo yote aliyoyasema Yesu tayari yamekwisha tokea na Yesu amesema hayo yakishatokea ni mwanzo wa utungu(mathayo 24:28), utungu unaozungumzwa hapa ni wa mjamzito kutaka kujifingua mototo sasa mwanzo wa utungu maana yake ni kwamba tukiziona dalili hizo alizosema Yesu tujue mtoto Yesu yuko karibu kuzaliwa (yaani yuko karibu kurudi duniani).Ndugu yangu nakusihi sasa uyasome maneno haya kwa tahadhari kubwa usije ukalia na kusaga meno milele, asomae na ufahamu.
C) WATAKATIFU KUCHUKIWA NA KUUWAWA (Mathayo 24:9-11).
Watakatifu wamepita katika dhiki za kila namna na mauaji ya kupitiliza duniani mfano;Paulo na Sila walitupwa gerezani (Matendo16:16-24) na baadae sana Paulo alikatwa kichwa rumi (Ufunuo2:10),Isaya alikatwa kwa msumeno kidole kwa kidole hata akafa kwa jinsi damu ilivyokuwa ikimiminika(Waebrania11:35-38).Stefano alipigwa mawe hata akafa (matendo7:59-60).Petro alisulubiwa msalabani k**a Yesu lakini kichwa chini miguu juu(Yohana21:18-19)(2petro1;14).Ndivyo ilivyo wengi watasalitiana na manabii wengi wa uongo watatokea duniani na kudanganya wengi ,uwe makini ndugu yangu Mwenye sikio na asikie (ufunuo 2:7).
C)KUONGEZEKA KWA MAASI NA UPENDO WA WENGI KUPOA
(Mathayo 24;12-13)
Maasi yameongezeka duniani, na maasi yanayozungumziwa hasa kwenya maandiko ni ya ulawiti na uasherati.Ulawiti umetokea duniani kwa namna ya kutisha,wanaume kwa wanaume kuoana(Ufunuo 22;15) katika lugha ya kibiblia neno mbwa linamaanisha shoga(kumbukumbu 23;18) ndoa za wengi zimevunjika kwasababu ya mume kutaka kumlawiti mkewe.Uasherati wa kutisha unatokea nyakati hizi.Si ajabu kwa mwanamke kuwa na mahawara hata 6 wakati ana mume na kwa tendo hilo wanamke huyo akajisifu kwa wenzake.Uasherati umekaribishwa hata katika familia,watoto wanaruhusiwa hata kuwa na wapenzi na wazazi wakafurahia.Na upendo wa wengi kupoa maana yake upendo wa kumpenda Yesu utapungua .Kumpenda Yesu huambatana na kushika maagizo yake (Yohana 14;23)(1Yohana 5:2-4)Lakini leo wako hata wachungaji wazinzi kwa namna ya kutisha upendo wao kwa Yesu sio tu umepoa lakini umekwisha kabisa,Bwana asifiwe mdomoni lakini moyoni hamna kitu.Lakini kwa habari ya watakatifu wanaoteseka Yesu amesema mwenye kuvumilia mpaka mwisho kuyakabili mateso hayo ikibidi hata kufa(Ufunuo 2:10)huyo ndiye atakaye okoka yaani huyo ndiye atakaye salimika kuingia katika moto wa milele (Mathayo 24:13).
E)INJILI KUHUBIRIWA ULIMWENGUNI KOTE (Mathayo 24:14)
Nyakati hizi za mwisho watu wengi wanadangnyika sana,wanatenda dhambi za kila namna wakitegemea kuwa Yesu hawezi kurudi sasa hivi kwa kuwa wanajua haji mpaka injili ihubiriwe ulimwenguni kote.Ni vema watu wote tuelewe kwamba injili ilikwisha hubiriwa ulimwenguni kote katika nyakati za kanisa la kwanza (Matendo 17:6). Kwa hiyo Yesu anaweza kurudi wakati wowote, Na taarifa sahihi kuhusu injili zinasema kuwa tangu mwaka elfu mbili (2000)na hata kabla ya hapo injili imezagaa karibu kila eneo la dunia.Kwa hiyo Yesu wakati wowote yuko mlangoni ,tubu leo dhambi zako ndugu yangu usije ukaachwa na kutupwa jehanamu ya moto milele na milele (asomae na afahamu ).Baada ya dalili hizo na nyingine kadha wa kadha ndipo litafuata tukio zito na la kutisha sana ambalo linaitwa,
2) KUNYAKULIWA KWA KANISA (1Wathesalonike 4:16).
Kila aliyeokoka anapaswa kulielewa somo hili kwa undani mno ili ajiweke tayari kunyakuliwa na Yesu na hata ambaye hajaokoka achukue tahadhari ya kuokoka na kukaa katika utakatifu ili naye asiachwe. Baada ya dalili hizo zote Yesu kristo atakuja kuchukua kanisa lake, wakati atakapokuja atakuwa angani sana kiasi cha kuto kuonekana na hata kanyaga chini k**a wengine wanavyofundisha na wanavyofahamu. Kunyakuliwa kutakuwa kwa gafla mno na kuwaacha watu wa dunia wakiwa wamepigwa na butwaa na kutokujua la kufanya, ni kwa mfano wa mwewe anavyonyakuwa kifaranga cha kuku na kumuacha kuku akiwa amepigwa na butwaa na hawezi kukipata tena kifaranga chake. Kwa namna hiyo watu waliookoka na kukaa katika utakatifu hadi dakika ya mwisho Yesu atakaporudi watapaa kwenda kumlaki mawinguni na kwenda nae mbinguni. Sasa wakati Yesu atakapokuja kuchukua kanisa lake kutatokea tukio zoto, tukio hilo ni lipi na litatokea kwa namna gani?. Twende pamoja katika kipengele kinachofuata.
(3)UFUFUO WA WAFU (Yohana 11:23,25).
Ufufuo huu wa wafu utatokeaje? Ni hivi, wakati Yesu kristo anakuja kunyakua kanisa wale waliookoka na kukaa katika utakatifu hadi dakika ya mwsho walipokufa walikwenda mbunguni. Sasa wakati wa Yesu kuja duniani watakatifu hawa waliokwenda mbinguni huirudia miili yao waliyokuwa nayo duniani na kufumba na kufumbua watabadilishwa miili yao wote na kuvalishwa miili mingine ya utukufu na kwa pamoja wataungana na watakatifu waliopo duniani walio badilishwa miili yao tayari na kupaa pamoja kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni pamoja (1Wathesalonike 4:13-17) (1Wakoritho 15:50-54) watakatifu waliopo duniani watanyakuliwa kwa namna hii – wengine watakuwa shambani, mmoja aliyeokoka na kukaa katika utakatifu hadi dakika hiyo atatwaliwa na huyu mwingine ambaye hajaokoka ataachwa na k**a wote walikuwa wameokoka na kukaa katika utakatufu hadi dakika hiyo wote watatwaliwa kwa pamoja (mathayo 24:40-41) watu watakuwa katika mambo yao na kufumba na kufumbua unyakuo utatokea, wengine watakuwa kwenye uzinzi, wengine baa, wengine wanapigana wengine wamelala nk. Lakini unyakuo utatokea papo hapo. Walio mbinguni watafufuliwa na kuungana na hawa waliopo duniani. Sasa ni vema tujue kuhusu aina za ufufuo.
AINA MBILI ZA UFUFUO
Kuna aina mbili kuu za Ufufuo wa wafu:
1) Ufufuo wa kwanza au ufufuo wa uzima.
2) Ufufuo wa hukumu au ufufuo wa aibu na kudharauliwa.
i) Ufufuo wa kwanza au ufufuo wa Uzima (Yohana 5:29).
Ufufuo huu unapewa majina mengine pia katika Biblia – Ufufuo ulio bora au Ufufuo wa wenye Haki(Yohana5:28-29)(Ufufuo20:4-6)(Luka14:13-14)(1Thesalonike4:16)(Ebrania11:35).Ufufuo wa kwanza unajumuisha wale wote waliokufa na kwenda mbinguni yaani wenye haki au watakatifu.Hawa ndio wenye sehemu katika ufufuo huu,watakuwa katika uzima wa milele katika mbingu mpya na nchi mpya. Huu ndio ufufuo ulio bora. Ufufuo huu uko katika sehemu mbili.
i)Ufufuo wa watakatifu wote walio mbinguni ambao watafufuliwa wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa.Hawa watafufuliwa kwanza kisha kufumba na kufumbua miili yao itabadilishwa na kuungana na wale walio hai ambao nao miili yao itabadilishwa na kuwa ya utukufu kisha wote kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana mawinguni(1 Wathesalonike 4:13-16).
ii)Ufufuo wa watakatifu wa wawakati wa dhiki kuu,hawa ni Waisraeli ambao hawakumsujudia Yule mnyama yaani mpinga kristo wala sanamu yake na kukataa kabisa kupokea chapa ya 666 katika vipaji vya nyuso zao. Na hivyo kukatwa vichwa na kuuawa kwa ajili ya Ushuhuda wa Yesu na Neno la Mungu waliokuwa nao wakati wa dhiki kuu, Hawa watafufuliwa wakati wa kuja kwa Yesu kristo mara ya pili pamoja na watakatifu wake walio nyakuliwa.Waisrael hawa baada ya kufufuliwa huku,moja kwa moja watatawala pamoja na kristo miaka elfu duniani(Ufunuo20:4-6)Wasraeli ndio wanaopewa onyo la kukwepa mahusiano yoyote na makristo wa uongo na manabii wa uongo,(Mathayo 24:23-27).Watakaofaulu kufanya hivi kwa kuwa na ushuhuda wa Yesu kuwa ndiye kristo mioyoni mwao hata wakifa katika dhiki hiyo,watafufuliwa katika ufunuo huu wakati huo
Sasa katika kipengele (i) watakatifu wata paa na kwenda kwa Yesu mbinguni,watakwenda mbinguni kupewa ijara au ujira wao kulingana na kazi ya Mungu walioitenda wakiwa duniani na kwa pamoja watakiendea kipindi kiitwacho
Taji kwa watakatifu na harusi ya mwana kondoo (Ufunuo19:9)(Mahayo2:4;26:26-29)
Kipindi hiki kitakachofanyika mbinguni kwa muda wa miaka saba (7) Na hapa duniani kitakuwa kipindi kizito kiitwacho Dhiki kubwa au Dhiki kuu ambacho namna yake haijawahi kutokea duniani wala haitakuwepo kamwe. Dhiki hii itakuwa ni ghadhabu ya Mungu kwa wote wenye dhambi (Mathayo 24:21)(1Wathealonike 1:10) na kipindi hiki cha dhiki kuu kitachukua muda wa miaka saba (7) (Daniel 9:27). Sasa kwa undani sana tuzame katika somo hili ili tujue nini kitakachofuata katika kipindi hiki kizito kiitwacho dhiki kubwa au dhiki kuu.
3) DHIKI KUBWA (Mathayo 24:21).
Baada tu ya kunyakuliwa kwa kanisa, Dhiki kubwa au dhiki kuu, itafuanika dunia nzima. Wote walioachwa, watakuwa katika kipindi hiki cha dhiki kubwa. Hii itakuwa ni pamoja na wote ambao hawakukubali kuacha dhambi na wale ambao walikuwa vuguvugu – kwa Yesu wapo na kwa Shetani wapo, yaani wale wote walioishi bila kushika maagizo yote ya Mungu yaani maneno yote ya Mungu yaliyo katika biblia nzima hawa pia watakaa na kupata mateso katika kipindi hiki cha dhiki kuu(zaburi 119:6). Ni muhimu sana kujifunza kwa undani juu ya kipindi hiki cha hatari ili tujihadhari na kuhakikisha hatuwi miongoni mwa watakaoachwa. Tukiliangalia somo letu.
Katika vipengele saba:-
(1) Dhiki kali kupita zote
(2) Muda wa dhiki kubwa
(3) Majina yanayotumika kuizungumzia dhiki kubwa
(4) Watakaohusika kuileta dhiki kubwa
(5) Makusudi ya dhiki kubwa
(6) Hali itakavyokuwa wakati wa dhiki kubwa
(7) Jinsi ya kuikwepa dhiki kubwa.
1) DHIKI KALI KUPITA ZOTE (Mathayo 24:21)
Wanadamu wanapita katika dhiki za kila namna katika dunia. Tangu zamani vizazi hadi vizazi kumekuwa na taabu,dhiki na mateso mazito kwa wanadamu vilio na majonzi yakutisha,karne kwa karne miaka kwa miaka na maumivu ya kila namna yamezingila katika dunia, hata kwa waliookoka yametokea hayo. Dhiki kwa waliookoka inaweza ikawa kupigwa na mume au hata kuachwa na mume, kukataliwa na wazazi, kunyimwa fedha za matumizi na wazazi au hata kutengwa kijamii. Yesu kristo alijua kwamba mtu aliyeokoka atapata dhiki, akasema,“Ulimwenguni mnayo dhiki;lakini jipeni moyo;“(Yohana 16:33)maandiko yanasema tumepewa siyo kumwamini Yesu tu ila na kuteswa kwa ajili yake(Wafilipi 1:29). Hata hivyo, dhiki ya watu waliookoka leo inaitwa “Dhiki Nyepesi” (2Wakoritho 4: 17) ukilinganisha na dhiki kubwa(Yoeli 2:11).Dhiki kubwa itakuwa haina mfano wake tangu kuumbwa kwa ulimwengu hata mwisho wake (Mathayo 24:21)(Daniel 12:1)
2) MUDA WA DHIKI KUBWA.
Dhiki kubwa itakuwa kwa muda wa juma moja la Daniel (juma la sabini – Daniel 9:24 – 27). Katika unabii wa Daniel, juma moja humaanisha miaka saba (Angalia Mwanzo 29:27). Nusu ya juma hili ni nusu ya miaka saba yaani miaka mitatu na nusu 3½ (au miezi 42 au siku 1,260).Miaka mitatu na nusu ya mwisho wa kipindi hiki, itakuwa ya kutisha sana kwa Waisraeli baada ya mpinga Kristo kuvunja agano nao (Ufunuo 11:2 -3)(Ufunuo 12:6(Ufunuo 13:5).
3) MAJINA YANAYOTUMIKA KUIZUNGUMZIA DHIKI KUBWA.
Ghadhabu itakayokuja. (1Thesalonike 1:10).
Saa ya hukumu (Ufunuo 14:7).
Adhabu (Isaya 24:21)(Isaya 26:21).
Saa ya kujaribiwa (Ufunuo 3:10).
Taabu yake Yakobo (Yeremia 30:7).
Uangamivu (Yoeli 1:15).
Siku ya giza na weusi,siku ya mawingu na giza kuu (Yoel 2:1-12).
4) WATAKAOHUSIKA KUILETA DHIKI KUBWA.
Dhiki hii itakuwa kubwa mno kutokana na watatu watakaohusika kuileta kwa wanadamu:-
Mungu – Mungu atahusika kikamilifu kuleta ghadhabu na mapigo makuu mno juu ya wote walioachwa (Isaya 26:21)(Yoel 1:15)(Ufunuo 14:7) (Ufunuo 15:17).
Shetani – Shetani atawashukia watu walioachwa kwa ghadhabu nyingi akijua wakati wake umezidi kuwa finyu mno wa kutupwa katika ziwa la moto milele na milele. (Ufunuo 12:12:).
Mpinga kristo – Biblia inasema Mpinga kristo pia anaitwa Mpingamizi, Asi Chukizo la Uharibifu au Mnyama(2Thesalonike2:1-8)(Mathayo 24:15)(Ufunuo 13:1-6).Katika (ufunuo 13:1-6), tunaona juu ya mnyama atokaye katika bahari na pia afananae na chui pia na miguu yake ilifanana na dubu na kinywa chake k**a kinywa cha simba sifa hizi zote za kinyama atakuwa nazo mpinga kristo,tunajua juu ya ukatili wa chui anavyoweza kumrarua mnyama kwa ghafla,dubu pia ni mkali mno,sasa ukali huo wa dubu utakuwa ndani ya mpinga kristo na ukali wa simba utakuwa ndani ya mpinga kristo na ukatili usioelezeka utakuwa ndani ya mpinga kristo. Sasa tuliona juu ya mnyama atakae katika bahari sasa nivema tujue maana ya neno habari katika maandiko.
TAFSIRI SAHIHI YA NENO BAHARI KATIKA MAANDIKO (Ufunuo 13:1).
Neno bahari katika maandiko ya unabii inawakilisha watu au mkutano mkubwa wa watu (Ufunuo 17:15)(Isaya 17:12;57:20). Mnyama anayetoka katika bahari ni mtu au mwanadamu (Ufunuo 13:18)anayetoka miongoni mwa watu wengi.
TAFSIRI YA VICHWA, PEMBE NA VILEMBA KATIKA MAANDIKO (Ufunuo 13:-6).
Vichwa,pembe na vilemba,ni alama ya nguvu na utawala(Ufunuo17:3,9-13). Mtu huyu au mnyama atakuwa amepewa uwezo na shetani mwenyewe na atafanya yote chini ya usimamizi wa shetani(Ufunuo13:4).Kutokana na ishara za mpinga kristo na mateso yake atawafanya watu wengi walioachwa kumwabudu shetani au wasipo muabudu watauawa(Ufunuo13:13-17) ili litimie neno la Yesu Kristo katika (Yohana 5:43).
5) MAKUSUDI YA DHIKI KUBWA.
(a) Kuliandaa Taifa la Israeli kumpokea Yesu k**a masihi wao pindi atakaposhuka kutoka mbunguni na watakatifu wake (Kumbukumbu 4:30-31)(Yeremia 30:7) (Ezekiel 20:37)(Warumi 11:25) Mungu alikwsisha kujifunga katika neno lake kuwa Israeli wote hawataangamia,na mpaka sasa waisraeli waliookoka ni wachache mno Duniani,na waisraeli wote waliobaki duniani wanaamini Yesu kristo hajaja na hivyo bado wanamsubiri Yesu aje duniani.
(b) Kuleta hukumu ya adhabu juu ya wote ambao hawakukubali wokovu(Isaya 26:20-21) (Thesalonike2:7-12).Mateso mazito yatakuwa yanawashukia wenye dhambi wote waliobaki duaniani.
6) HALI ITAKAYOKUWA WAKATI WA DHIKI KUBWA.
Wakati wa dhiki kubwa kutakuwa na mateso na dhiki isiyoelezeka.Itakuwa ni kilio na kusaga meno kwa wale walioachwa. Watu watauwawa na damu yao kumwagwa k**a mavumbi na nyama yao k**a mavi wala hawatakuwepo watu wa kuwalilia wala kuwazika (Sefania 1:15,17-18)(Yemia25:33)(Isaya26:21).Leo watu wanatenda dhambi na inaonekana k**a Mungu hayupo.Hasira yake yote imewekwa akiba na itafunuliwa wakati wa dhiki kubwa (Sefania 2:1-3).Wachungaji na Wainjilisti ambao hawakukubali kuokoka na kuishi katika utakatifu na wanawapoteza watu watakuwepo kwenye mateso hayo(Isaya 24:1-6). Itakuwa ni dhiki kubwa(Isaya24:17-18).Watu wataiambia milima iwaangukie iwasitiri,milima haitafanya hivyo(Ufunuo6:15-17).Watu watakuwa katika maumivu mchana na usiku wakikinywea kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya Mungu isiyochanganywa na maji (Ufunuo 14:9-11) Watu watatamani kujiua, lakini mauti ya namna hiyo haitakuwepo,mpaka wateswe na kuuawa sio kujiua kwa matakwa yao(Ufunuo 9:2-6).Mapigo ya Mungu yatatimizwa kwa kumwangwa kwa mapigo saba ya kutisha juu ya wanadamu (Ufunuo 15:1:16:1-6,8,21)
PIGO LA KWANZA.(Ufunuo 16:1-2).
Majipu mabaya naya kutisha juu ya watu waliobaki katika uso wa nchi.
PIGO LA PILI (Ufunuo 16:3).
Ghadhabu ya Mungu itamwagwa juu ya bahari na bahari yote itakuwa damu k**a damu yamfu na viumbe vilivyo hai vyote katika bahari vitakufa.
PIGO LA TATU (Ufunuo 16:4).
Chemchemi za maji kuwa damu.
PIGO LA NNE (Ufunuo 16:8-9).
Jua litawaunguza watu hakuna mfano wake kwa moto wa kutisha.Wenye mafunuo wengine husema kuwa maumivu hayo yatatokana na kuwa jua litashushwa chini sana na kuwatesa sana watu kwa mionzi mikali ya jua hakuna mfano wake, kutokana na hilo watu watamtukana Mungu kwa sababu watamuomba Mungu lakini Mungu hatasikia maombi yao na kwa sababu hiyo hawatatubu bali watakufuru.
PIGO LA TANO(Ufunuo 16:10-11).
Mapigo juu ya kiti cha enzi cha mpinga kristo na ufalme wake kwa ujumla.Na hao wote watamtukana Mungu kutokana na maumivu mazito.
PIGO LA SITA (Ufunuo 16:12).
Maji ya mto frati kukauka.
PIGO LA SABA (Ufunuo 16:17-21).
Umeme na sauti za radi na tetemeko zito lisilo na mfano wake tangu wanadamu waanze kukaa juu ya nchi.Visiwa vitakimbia na milima haitaonekana tena na mvua kubwa mno ya mawe itashuka kutoka mbinguni ikiwashukia wanadamu.Wanadamu watamtukana Mungu mno kutokana na mapigo hayo.Kutokana na taabu watakayopata,wanadamu watamwomba Mungu ili awahurumie,lakini huruma ya Bwana itakuwa imekoma(Isaya 26:16-18).Katika miaka 3½ ya iliyosalia chukizo la uharibifu litasimama kikamilifu juu ya Taifa la Israeli(Danieli 9:27). Ghadhabu juu ya Israeli itakuwa kubwa mno kiasi cha kuwafanya Waisraeli waikimbie nchi yao (Mathayo 24:15-16-22).Wateule wanaotajwa hapo siyo sisi tuliookoka leo.
Neno “Mteule” au “Wateule” linatumika katika Biblia kwa maana nne tofauti.
1. Yesu kristo (Isaya 42:1)
2. Malaika Watiifu (1Timotheo 5:21)
3. Sisi tuliookoka (Tito 1:1)(1 Petro 1:1-2)(Warumi 8:33)(Luka 18:7)
4. Taifa la Israeli(Isaya 65:8-9)(Isaya 45:4) wateule katika (mathayo 24:21 – 22), ni taifa la Israeli.
7) JINSI YA KUIKWEPA DHAKI HII KUBWA.
Kila anayetaka kuikwepa dhiki hii kubwa inambidi kujificha ndani ya vyumba na kufunga mlango k**a wakati wa Safina ya Nuhu (Isaya 26:20), kwa kufanya ya kufatayo:-
Kuhakikisha ametubu dhambi na kuziacha na kuokolewa kwa kumwamini mwana wa Mungu Yesu Kristo (Mithali 28:13)(Yohana 3:16).
Kukaa ndani yake Yesu kwa kufuata neno lake na maagizo yake yote kwa gharama yoyote, siyo kukaa ndani ya mapokeo ya wanadamu au mpokeo ya dhehebu (1Yohana 2:28)(Zaburi 119:6,9)
Kukaa mahali ambapo pana waalimu wenye mafundisho yote ya kweli ili tujue yote ya kutenda na kutokutenda (Isaya 30:20 – 21)
Kukesha wakati wote kwa kuyatunza mavazi meupe yaani utakatifu. Doa dogo tu husababisha uchafu(Ufunuo16:15).Mbweha wadogowadogo yaani dhambi tunazoziona ndogo ndogo zitatufanya tuachwe (Wimbo ulio bora 2:15) sasa tukifanya haya yote hakika hatuwezi kuachwa tutakwenda pamoja na Yesu mbinguni katika kipindi kiitwacho taji kwa watakatifu na harusi ya mwanakondoo. Sasa tuangalie kwa undani yatakayofanyika katika kipindi cha taji kwa watakatifu na harusi ya mwana kondoo baada tu ya watakatifu kwenda na Yesu mbinguni.
(1) TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO.
Tuliona katika somo la kunyakuliwa kwa kanisa jinsi ambavyo watakatifu watakavyonyakuliwa wote kwa pamoja – wale waliookoka na wapo mbinguni watarudi katika miili yao kwa ufufuo na sisi tuliopo sasa baada ya kubadilishwa miili yetu kufumba na kufumbua tutaanza kwenda mawinguni kwa kupaa na kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni. Sasa tuangalie yatakayofuata mara tutakapopaa na kwenda na Yesu mawinguni katika vipengele vifuatavyo:-
Kuondoka kwa Shangwe kwa watakatifu.
Kiti cha thawabu au taji.
Kujaribiwa kwa kazi ya kila mtu.
Aina za taji zitakazotolewa kwa watakatifu.
Harusi ya mwanakondoo.
KUONDOKA KWA SHANGWE KWA WATAKATIFU
Wakati wa kuondoka, kwa muda mfupi sana tutafundishwa nyimbo mbili na Mungu mwenyewe.Wimbo mmoja unaitwa wimbo wa Musa na mwingine wimbo wa mwanakondoo (Ufunuo 15:3-4).Mungu alimfundisha wimbo Musa na kumwambia awafundishe Waisraeli ili waukumbuke wakati Mungu atakapowaka hasira juu yao na kuwaacha(Kumbukumbu 31:17-19) (Kumbukumbu 32 yote).Hiki kilikuwa kivuli cha mambo yajayo wakati tutakapoimba Wimbo wa Musa na kuondoka huku nyuma yetu hasira ya Mungu ikidhihirika kwa wenye dhambi waliobaki wakati wa dhiki kuu (Wakosai 2:17). Vile vile, Musa na wana wa Israeli baada ya kuwaona Wamisri wamekufa baharini, na kutenganishwa nao kabisa (Kutoka 15:1 – 20). Sisi nasi itakuwa vivyo hivyo, Tutaimba wimbo wa Musa tutakapoanza kutenganishwa na watenda dhambi huku wakipata mateso duniani wakati tunakwenda Kaanani (yaan mbinguni). Siyo hilo tu Yesu Kristo alikuwa akiimba kwa kumshinda Shetani pale msalabani, Yesu alishangilia kwa wimbo (Wakolosai 2:14-15). Wimbo huu ndio wimbo wa Mwanakondoo. Tutauimba tukiwa tunapaa juu mawinguni baada ya kumshinda shetani na majaribu yake yote.
KITI CHA THAWABU AU TAJI
Bibilia inataja mara kwa mara kwamba kutenda kazi kwetu katika wokovu kutazawadiwa.Tutapewa taji au thawabu (Ruthu2:12)(Zaburi 58:11) (Mathayo 13:13;23)(Isaya 40:10;49:3-4)(Yeremia 31:16)(Mathayo 5:12;10;41)(1Wakoritho 3:8;9:25;15:58)(Waebrania 10:35)(2Yohana 1:8).Thawabu hizi au taji hizi atakuja nazo Yesu mawinguni na kila mmoja atalipwa kulingana na utumishi aliomfanyia Mungu katika kipindi chake cha wokovu, na zitatolewa mawinguni mara tu baada ya kumlaki Yesu (Ufunuo 22:12)(2 Timotheo 4:8)(Luka 14:12 -13). Yesu atakalia kiti kinachoitwa KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO wakati wa kutoa taji (2 Wakoritho 5:10)Kiti hiki atakalia Yesu na kutoa hukumu kwamba nani apewe thawabu ipi au taji ipi. Tungeweza kukiita kiti cha thawabu au taji.
KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU
Wakati wa BEMA, kazi ya kila mtu aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia Mungu itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika thawabu ipi atakayoipata (1 Wakoritho 3:12-15).Moto huu ni Mungu mwenyewe na Yesu Kristo kwa kuwa Baba na Mwana wa moja (Yohana 10:30) kwa hiyo k**a Baba ni moto Mwana pia ni moto (Kutoka 24:17)(Isaya 33:14) (Waebrania 12:29). Kazi ya kila mtu itajaribiwa kwa kulinganishwa na jinsi ambavyo Yesu Kristo mwenyewe angeifanya kazi hiyo kwa karama hizo hizo alizopewa mtu Yule ingekuwaje?.
AINA ZA TAJI ZITAKAZOTOLEWA KWA WATAKATIFU
Haitapendeza kabisa kumwona mtu ambaye hakupewa taji yoyote wakati alikuwa na muda wa kumfanyia kazi Mungu tofauti na yule mhalifu msalabani. Ni wajibu wetu kuwa na lengo la kupata taji zozote zifuatazo. Kwa gharama yoyote katika maisha yetu ya wokovu.
TAJI ISIYOHARIBIKA (Wakoritho 9:23-25)(2Timotheo 2:4-6).
Taji hii watapewa watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya injili ili kuishiriki pamoja na wengine. Walijizuia yote kwa utoaji wao kwa ajili ya Injili, walijizuia yote katika maombi kwa ajili ya Injili na pia Walitumia vyote walivyo navyo: muda, ujuzi, vipawa, vyeo vyao, uwezo wao wote nk. Ili kuishiriki injili pamoja na wengine.
TAJI KUJIONEA FAHARI (1 Thesalonike 2:19)(Daniel 12:3).
Taji hii inaitwa taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaoipata taji hii watang’ara k**a nyota tofauti na wengine wakatavyong’aa, fahari yao itakuwa kubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale waliowaleta watu wengi kwa Yesu, utukufu wao utakuwa mkubwa kuliko wengine. Kutokana na kushuhudia kwao au kuhuburi. Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya mtu kwa mtu au vinginevyo na wakawaongoza mahali ambapo watakuzwa kwa mafundisho na kuwa watenda haki hawa watang’ara kwa namna ya kutisha.
TAJI YA HAKI. (2 Timotheo 4:7-8)
(a) Taji hii ni kwa wale waliopenda kufunuliwa kwake Yesu Kristo wakati wote moyoni walisema “Amina; na uje Bwana Yesu”. Walikuwa katika utakatifu wakati wote. Kila neno walilojifunza walilitendea kazi. Kwao hakukuwa na kurudirudi nyuma yaani kuuacha wokovu halafu kurudia wokovu. Watu wa namna hii ambao hawakuuacha wokovu mpaka alipokuja Yesu akawakuta katika hali ya kutubu wataipata taji hii.
TAJI YA UTUKUFU ILE ISIYOKAUKA
(1Petro 5:2-4)(Mathayo 10:41-42)
(a) Taji hii watapewa Wachungaji,Waalimu au Watumishi wa Mungu wanaojitaabisha kuwafundisha wengine na kuwalea kiroho kwa njia zozote,kuwafundisha Kanisani na kuwapa huduma za kichungaji kuandika vitabu au Tract au maandishi yoyote yanayowasaidia watu wengine kiroho.
(b) Taji hii pia watapewa wale ambao wanatumia muda wao kuwafatilia watoto wachanga wengi wa kiroho mpaka wanakua. Namna yoyote ya kumsaidia mtu kujifunza neno, atapata thawabu hii. Kumuazima kaseti za neno ili akue kiroho, kumpatia nauli ili aende kwenye mafundisho, kazi ya kuhudumu kanisani,kuwafundisha watoto au kufanya lolote ili watu wawe na raha ya kujifunza neno
(c) Taji hii pia watapewa wale ambao wanahudumia mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu ili wapate urahisi wa kufanya kazi zao.
HARUSI YA MWANA-KONDOO.
Watu waliookoka wanaoishi katika utakatifu, wanaitwa BIKIRA SAFI WA KRISTO (2Wakoritho 11:2) na pia BIBI HARUSI WA KRISTO (Yohana 3:29). Basi baada ya kupewa taji, Yesu atatufanyia karamu kubwa kutupongeza. Hii ndiyo karamu ya Harusi ya Mwana-kondoo (Ufunuo 19:7-9). Hii itafanyika katika kipindi hichohicho cha miaka saba wakati huku duniani wako katika dhiki kuu na baada ya hapo kitafuata kipindi kiitwacho,
(6) KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI
Katika wakati huo Yesu pamoja na watakatifu wake pamoja na mwaliko mkubwa wa malaika,watashuka kutoka mbinguni kwa ajiri ya utawala wa miaka 1,000 duniani. Yesu atakuwa amepanda farasi mweupe akituongoza na sisi kila mmoja wetu atakuwa amepanda farasi mweupe tukimfuata maelfu kwa maelfu pamoja na malaika (Yuda 1:14)(Ufunuo19:11-14).Na Yesu atakuwa amezungukwa na mwali wa moto (1Thesalonike 1:7-8) na atakuja k**a umeme unaoonekana pande zote.Mara tu tutakapoanza safari jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni kwa lengo la kupamba sherehe ya kifalme. Nyota hizi ni zile zipitazo upesi mawinguni “VIMONDO” (Mathayo 24:29-30).Atakuja na kukanyaga Milima Mizeituni, mahali pale pale alipopaa kwenda mbinguni wakati alipotoka duniani mara ya kwanza(Matendo 1:10-12)(Zekaria 14:4-5).Wakati Yesu atakapokuwa anakuja duniani kwa ajili ya utawala wa miaka 1,000 pamoja na watakatifu wake, yatatokea matukio mengine. Matukio hayo ni yapi?. Twende pamoja katika vipengele vitatu vifuatavyo.
(7) KUKUSANYWA KWA WATAKATIFU KUTOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA.
Wakati Yesu atakapokuja yatafuata matukio matatu, ambayo ni kukusanywa kwa watakatifu kutoka pande zote za duania, ufufuo wa wafu kwa wana wa Israeli na vita vya har – magedoni. Maandiko hayaelezi waziwazi kuwa tukio lipi litakaloanza na lipi litakalofuata, lakini ni mambo ya muhimu mno kufahamu na kuzingatia japo kwa sehemu, kwa hiyo Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake atatuma malaika zake kwenda pepo nne za dunia ili kuwakusanya waisraeli walioikimbia dhiki kali katika kile kipindi cha miaka mitatu na nusu 3½ ya mwisho ya dhiki kubwa ili wasipotezwe na mpinga kristo na nabii wa uwongo kwa kukwepa kupata chapa ya mpinga kristo ya 666. Wale wote waliokwepa kupotezwa na mpinga Kristo na nabii wa uongo watakusanywa. Watakaokuwa wamekusanywa ni pamoja na waisraeli waliokufa na kufufuliwa mwishoni wa dhiki kubwa na waliuwawa kwa kukataa kumsujudia mnyama na kukataa kupokea chapa ya 666 na hivyo kukatwa vichwa vyao(Ufunuo20:23-27,29-31) na baada ya kukusanywa watakuwa wamechanganyika na watenda dhambi ambao ni mataifa na hivyo watabaguliwa na Yesu mwenyewe k**a mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi (Mathayo 25:31-34) maneno haya wanaambiwa wana wa Israeli ingawa tunaweza kuyatumia maandiko haya katika mahubiri yetu mbalimbali ya hukumu ya mwisho.Ni muhimu kukumbuka kuwa kuna fufuo mbili tu lakini katika hizo mbili ufufuo wa kwanza ni ufufuo kwa watakatifu uliogawanyika katika makundi mawili (a) Ufufuo wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa (b) Ufufuo kwa wana wa Israeli wakati wa Yesu kuja mara ya pili duniani. Ni muhimu kukumbuka kuwa fufuo hizi zote zipo katika ufufuo wa kwanza kwa ajiri ya watakatifu tu. Na baada ya hapo litafuata tukio jingine liitwalo,
VITA VYA HAR – MAGEDONI.
Baada ya hapo, itatokea vita itakayopangwa na shetani na majeshi yake ili kupambana na Yesu lakini Yesu atashinda kwa muda mfupi sana. Vita hiyo itajulikana kwa jina la VITA VYA HAR- MAGEDONI (Ufnuo 16:14,16). Vita hivi vitatokana na mpango wa Shetani wa kutaka kuchukua ufalme kutoka kwa Yesu kristo k**a alivyojaribu kuchukua ufalme kwa Mungu mbinguni (Ufunuo 12:7-8). Kwa jitihada za pamoja, shetani, mpinga Kristo (Mnyama) na Nabii wa uongo,watatuma roho chafu ambazo zitawaandikisha watu mataifa waliobaki katika dhiki kubwa kutoka duniani kote na kuwaweka tayari kwa vita, wataandikishwa na shetani ili kupigana na majeshi ya Yesu kristo mahali paitwapo kwa Kiebrania Har-Magedoni. Hapa ni bonde la Megido ambalo limekuwa mahali pa vita muda mrefu wa nyakati za zamani za biblia. Bonde hili lipo kusini magharibi mwa mlima wa KARMELI (2Nyakati 35:22)(Zekaria 12:11)(1Wafalme 18:17-19). Katika vita hiyo mpinga kristo na nabii wa uwongo watak**atwa na Yesu mwenyewe na kutupwa wangali hai katika ziwa liwakalo moto na kiberiti.Ziwa la moto kwa sasa halina mtu.Watenda dhambi wakifa sasa wanakwenda jehanum ya moto sio katika ziwa wa moto,kuna tofauti kati ya jehanamu ya moto na ziwa la moto na kwa hiyo katika vita vya har-magedoni kutakuwa na mauwaji mazito mno.Wenye dhambi watauawa kwa maangamizo yasiyoelezeka na damu za watu hao zitatiririka kiasi cha maili mia mbili (Ufunuo 17:12-14;14:19-20;19:11-21)(Isaya 13:9;29:5-8).Hapo tutamwona Yesu akiwa mtu wa vita na Bwana wa vita halisi (Kutoka 15:3). Ingawaje wenye dhambi watakufa lakini hawatakufa wote, kwa sababu hiyo watakuwepo watenda dhambi katika utawala wa miaka 1,000 wa Yesu na watakatifu wake duniani lakini hawatatenda dhambi, kwa sababu shetani mleta dhambi atakuwa amefungwa katika shimo refu sana kwa muda wa miaka 1,000 ili asiwadanganye mataifa na atafungwa mwishoni mwa vita hivyo,kwa hiyo kutakuwa hakuna ushawishi wa dhambi duniani.(Ufunuo 20:1-3). Na baada ya hayo litafuata tukio zito la furaha sana liitwalo,
(8) MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI.
Tulijifunza katika somo la “Kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili duniani na Jinsi ambavyo Yesu Kristo atakavyokuwa mtu wa vita au Bwana wa vita halisi. Yesu Kristo atawauwa weye dhambi wote waliojipanga kupigana naye mahali paitwapo kwa Kiebrania Har-magedoni. Wale wote watakaouawa hapa ndege watashiba nyama zao, kisha Yule mnyama (Mpinga Kristo) na Yule nabii wa uongo watak**atwa na kutupwa wangali hai katika Ziwa la mto (Ufunuo 19:20 -21). Baada ya tukio hili, shetani naye atak**atwa na kutupwa kwenye shimo refu (Ufunuo 20:1-3). Baada ya kufungwa shetani miaka 1,000 ndipo utawala wa Yesu Kristo duniani pamoja na watakatifu wake, utakapoanza (Ufunuo 20:4-6). Ni makusudi ya somo hili kujifunza kwa undani juu ya Utawala huu wa Yesu kristo wa miaka 1,000 duniani. Somo litakuwa na vipengele kadhaa vifuatavyo.
1. Makusudi ya utawala wa miaka 1,000 wa Yesu kristo duniani
2. Hali ya maisha itakavyokuwa wakati wa utawala wa Yesu kristo duniani
3. Vita vya Gogu na Magogu.
1) MAKUSUDI YA UTAWALA WA MIAKA 1,000 WA YESU KRISTO DUNIANI.
Mwanzoni kabisa katika mpango wa Mungu mwanadamu alikusudiwa kuishi maisha ya amani, furaha na mafanikio, chini ya utawala wa Mungu mwenyewe. Adamu alipotenda dhambi, aliukatisha mpango huu kwa mwanadamu na akatolewa katika bustani ya Edeni. Hapo ndipo maisha magumu kwa mwanadamu yalipoanza. Ardhi ililaaniwa na tukaanza kula chakula kwa jasho, na kuishi maisha ya taabu tofauti kabisa na mpango wa Mungu kwa mwanadamu(Mwanzo 3:16-19). Ndipo Mungu alipoanza mpango wa kumrudisha mwanadamu katika amani na furaha aliyomkusudia, na hatimaye akaja Yesu Kristo duniani mara ya kwanza na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Hata hivyo katika kukamilisha kile alichokikatisha Adamu, Mungu katika mpango wake amekusudia kuwaonesha kile alichokusudia kwa watu wake kwamba angewaweka katika maisha gani k**a Adamu asingetenda thambi,na kuugeukia utawala wa shetani. Na kwa kuwa shetani atakuwa amefungwa miaka elfu moja wanadamu wataweza kutawaliwa bila kushawishiwa na Ibilisi kutenda dhambi na kwa hiyo watu watakuwa katika serikali moja duniani kote, iliyo chini ya utawala wa Yesu kristo. Na wanadamu wenye dhambi waliomkataa Mungu awatawale waliotoka katika kipindi cha dhiki kubwa watakuwepo katika kipindi hiki. Na baada ya kuona wema huo wa Mungu utaleta mjuto kwao wakijua baada ya furaha hiyo yatakuja mateso mazito ya Milele.
NIMEISHIA HAPA
2) HALI YA MAISHA ITAKAVYOKUWA WAKATI WA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI.
• FURAHA ITAJAA KATIKA ULIMWENGU.
Hakutakuwa na huzuni wala masikitiko kabisa Ulimwenguni (Isaya 9:3-4)(Yeremia 31:13).
• UTAKATIFU UTATAWALA DUNIANI.
K**a kilivyokuwa kipindi cha waamuzi katika Agano la kale, watakatifu wanaotawala na kristo watakuwa ni waamuzi. Watawashauri watu na kuwahukumu kwa hekima kuu itakayoleta maisha ya uaminifu na yanayompendeza Mungu (Isaya 40:5)(Isaya 1:26).
• UTUKUFU WA BWANA UTAFUNULIWA.
Kila mtakatifu atakayetawala pamoja na Yesu kristo atakuwa katika utukufu mkubwa tofauti na wale wanatawaliwa (Isaya 40:5)(Isaya 35:2)(Isaya 11:10)
• UTAKUWA NI WAKATI WA FARAJA BAADA YA HASIRA.
Baada ya mapigo ya dhiki kuu na vita vya Har-Magedoni, muda huu utakuwa wakati wa faraja baada ya hasira (Isaya 12:1,54;7-10,40:11).
• UTAKUWA NI UTAWALA WA HAKI TUPU.
Utawala huu utakuwa ni utawala usio na uonevu kwa jinsi haki itakavyokuwepo (Isaya 9:7;11:5)(Yeremia 23:5;33:15).
• DUNIA ITAJAWA NA KUMJUA BWANA.
Kila mtu atamjua Mungu – Wema wake, uzuri wake, haki yake n.k. kila mtu atamjua Yesu kuwa ni Mungu na kujawa maarifa kamili ya mpango wake kwa mwanadamu (Isaya 11:9) (Habakuki 2:14).
• LAANA JUU YA ARFHI ITAONDOLEWA.
Laana iliyotajwa katika (Mwanzo 3:17-19) itaondolewa. Hakutakuwa na miiba wala magugu mvua itakuwa ya manyunyu safi. Ukilima kidogo unavuna sana hakuna kula kwa jasho (Ezekieli 34:26 -27).
• HAKUNA KUUGUA DUNIANI.
Magonjwa yote yanaletwa na shetani. Kwa kuwa shetani atakuwa amefungwa hakutakuwa na kuugua. Kwa hiyo Hospitali zitakuwa hazina kazi kabisa (Isaya 33:24)
• HAKUTAKUWA NA VILEMA, VIPOFU WALA VIZIWI DUNIANI.
Kazi zote hizi zilitokana na shetani kupewa nafasi ya kumawala Adamu kazi hizi zitamalizwa katika utawala huu. (Isaya 29:18)(Isaya 35:3-6).
• KUTAKUWA HAKUNA KUFA.
Watu watazaliwa tu, lakini hakuna kufa. Watu watakuwa wengi mno Duniani watakao kuwa wanaoa na kuolewa ni wenye dhambi, watakatifu hamu ya kuoa au kuolewa haitakuwepo (Amosi 9:15)(Zekaria 14:9-11).
• HAKUNA KUONA NJAA, KIU, WALA MATESO.
Nyakati hizo zitakuwa kuimba tu, hakuna jua kali wala baridi kali, wala mateso. (Isaya 49:10; 14:3-7).
• DUNIA ITAPENDEZA MNO NA HAKUTAKUWA NA UMASIKINI.
Kila sehemu kutakuwa na maua mazuri mno wala hakutakuwa na majangwa kabisa (Isaya 65:21 -24)(Isaya 35:1-2,7). Baada ya hayo yote kutatokea tukio jingine liitwalo,
• VITA VYA GOGU NA MAGOGU.
Mwishoni mwa miaka hii elfu, shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake na ataanza kuwadanganya watu wenye dhambi, watakatifu wa Yesu haiwezekani tena kushawishika kutenda dhambi. Kifupi waliookoka na kunyakuliwa na Yesu mawinguni katika kipindi cha kunyakuliwa kwa kanisa na wana wa Israeli waliotoka katika kipindi cha dhiki kuu na walio fufuliwa, hawa haiwezekani kamwe kwenda motoni milele. Shetani atawashawishi wenye dhambi ambao kwa wakati huo watakuwa wengi k**a mchaga kwa sababu wao walikuwa wanazaliana na hawafi na shetani atashawishi ili wafanye vita na kupigana na Yesu na watakatifu wake. Watu wote kwa kuwa wana asili ya dhambi watashawishika, na watajikusanya nchi ya Gogu na Magogu, iliyo kaskazini ya Palestina, Mashariki ya Kati, na kuja kuishambulia maskani kuu ya watakatifu Yerusalemu. Hapo ndipo itatokea vita vya Gogu na Magogu. Hasira ya Mungu itawaka na wanadamu wote wataangamizwa kwa kuliwa na moto utakaoshuka kutoka mbinguni. Watabakia watakatifu pamoja na Yesu tu. Shetani naye atak**atwa na kutupwa katika Ziwa la moto (Ufunuo 20:7-10).. wale wote walioliwa kwa moto watakwenda wote Jehanamu yam to kusubiri ufufuo wa pili, au ufufuo wa hukumu.
• UFUFUO WA PILI AU UFUFUO WA HUKUMU.
Ufufuo huu pia unaitwa Ufufuo wa aibu na kudharauliwa (Yohana 5:28-29)(Daniel 12:2). Huu ni ufufuo wa watenda mabaya na wenye dhambi wote, ambao watakuwa wanatoka Jehanamu ya moto. Wote walioko Jehanamu hivi sasa na wote wenye dhambi tangu vizazi vya mwanzoni kabisa vya Adamu hadi wale watakaokufa na kwenda motoni katika vita vya Gogu na Magogu (Ufunuo 20:7-9) watafufuliwa na watakapokuwa wanafufuliwa watairudia miili yao ya asili yaani miili ya duniani na baada ya kufufuliwa Yesu ataketi ili ahukumu. Atakalia nini, atahukumu vipi na atatumia nini kuhukumu? Twende pamoja katika vipengele vifuatavyo.
(9) KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU.
Mara tu baada ya wenye dhambi kufufuliwa Yesu kristo muhukumu wa haki atakalia kiti cheupe ili aweze kuhumumu. Watu walipokwenda motoni walikuwa hawajaelezwa waziwazi makosa yao yaliyowapeleka motoni sasa hapa ndipo mahali ambapo Yesu Kristo muhukumu wa haki atakapowaonesha waziwazi matendo yao kwa mfano wa video (Ufunuo 20:5,11-15). Itakuwa ni aibu mno na kudharauliwa maana siri zote za mtu zitakuwa wazi, yote aliyoyafanya ya uzinzi akiwa sirini yataoneshwa waziwazi mbele ya watu wote. Hapa watu watajitetea “Bwana Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina la jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? “naye Yesu atawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu (Mathayo 7:22 – 23) Wote watatupwa kwenye ziwa la moto, sasa ili tuenlewe yale yatakayofanyika hapa tutaligawa somo letu katika vipengele saba:-
1. Hakimu yupi atakaye kikalia kiti cha hukumu siku ya mwisho?
2. Makusudi ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe.
3. Wingi wa watu watakaohukumiwa.
4. Wadogo pia kuhukumiwa.
5. Kipimo kitakachotumiwa katika hukumu.
6. Kufunuliwa kwa siri zote mbele ya mashahidi wa Mungu.
7. Hukumu ya mwisho.
(1) HAKIMU YUPI ATAKAYE KIKALIA KITI CHA HUKUMU SIKU YA MWISHO.
Hakimu atakayekikalia kiti hiki ni Yesu Kristo. Yeyote leo anayemkana Yesu Kristo kuwa siyo mwana wa Mungu, atafahamu hapa kuwa hukumu yote iko chini yake (Yohana 5:22)(Matendo 10:38 -42)(Warumi 2:16)(2 Timotheo 4:1). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari kuturehemu na kutusamehe kabisa (Isaya 55:6-7). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa (Ezekiel 7:4;18)(Warumi 2:4-5).
(2) MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE.
Hukumu hii, haitakuwa na makusudi ya kuwaweka huru wenye dhambi, k**a wengine wanavyodhani. Ilivyo ni kwamba yeyote Yule asiyemwamini Yesu hadi kufa kwake ghadhabu ya Mungu inamkalia (Yohana 3:36). Mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa huenda motoni moja kwa moja (Luka 16:19-24). Mtu huyu huenda huko bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mates ohayo. Makusudi ya hukumu hii itakuwa kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya Jehanamu uhalali wa yeye kupewa adhabu hiyo ya milele. Itadhihirishwa kwa kila mmoja mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyopaswa kuyapata kwa kadri ya matendo yake aliyotenda duniani (Matendo 17:31)(Warumi 2:6).
(3) WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA.
Watu wanaokwenda Jehanamu ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikiria (Mathayo 7:13-14). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbali mbali, kitabu cha uzima ambamo huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya Mungu (Luka 10:20)(Wafilipi 4:3). Wale waliookoka wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao, na kuondolewa katika kitabu cha uzima (Kutoka 32:33)(Ufunuo 3:5). Wale wote watendao dhambi ambao hawakuukubali wokovu majina yamo katika vitabu vya kumbukumbu vitabu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yako katika Vitabu Vingi lakini wale wa mbinguni wako katika “Kitabu kimoja cha uzima (Ufunuo 20:12) kwa kuwa ni wachache. Hatupaswi kudanganyika kutokana na watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza wote duniani na kuwabakisha watu 8 tu walio watakatifu na Mungu wetu habadiliki (Waebrania 13:8) hata leo ndivyo alivyo bila utakatifu wa mwili na roho haiwezekani kumuona Mungu (Waebrania 12:14;1)(Wakorintho 7:34)(Mathayo 5:48).
(4) WADOGO PIA KUHUKUMIWA.
Wakubwa kwa wadogo, watakuwepo kwenye hukumu hii (Ufunuo 20:12). Ni muhimu kuwashuhudia Injili watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya, na kuwapa nafasi ya kutubu na kuokolewa au sivyo tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii wakiwa wametoka kwenye mateso ya Jehanam ya moto na kusubiri hukumu ili watupwe katika ziwa la moto. Mtoto mdogo anayeweza kufahamu hesabu ya 59+68 anaupeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika Injili yetu kwa watoto wa jinsi hii tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa wizi wa kalamu, uongo, kutowatii na kuwaheshimu wazazi n.k. Baada ya mtoto kumwamini Yesu, mwongoze sala ya toba. Baada ya hapa, fahamu kuwa ameokoka na endelea kumfundisha bila kubabaishwa na mambo ya kitoto anayoyafanya siku kwa siku. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasiofahamu sheria ambao ufalme wa Mungu ni wao. Wengi wao huwa bado wana umri kukumbatiwa (Marko 10:13-16; (Warumi 4:15,5:13).
(5) KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.
Watu wengi wanafanya makosa makubwa pale wanapofikiria kwamba, watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sawa na mafundisho ya madhehebu yao au wachungaji wao. Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu katika hukumu. Wengi wanajifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachunga wao au madhehebu yao, ingawa yako tofauti na maagizo ya Neno la Mungu hawa wote watakwenda katika hukumu ya mateso yam to wa milele. Kipimo atakachotumia Yesu katika hukumu ni Neno la Mungu au Injili (Warumi 2:16). Ni muhimu kuyalinganisha yale tunayoyafanya na neno la Mungu na siyo mafundisho ya madhehebu yetu au wachungaji wetu au maaskofu wanaotuambia kufanya hili au lile siyo lazima (Zaburi 119:6,9). Siyo hilo tu kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa neno la Mungu. Wale ambao hawakuwa na Biblia kijijini kwao, wale ambao walikaa mahali kusipokuwa na mafundisho, wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa Wakristo, wote hawa watapotea pasipo kuifahamu sheria (Warumi 2:12). Kukosa kufahamu yaliyo halali, siyo udhuru utakaokubalika (luka 12:48). Bado wasiojua mapenzi ya Mungu watakwenda motoni. Wale wanaofahamu mafundisho lakini hawayatendi wao pia wataangamia pamoja na kuyajua hayo (Mambo ya walawi 5:17)(Warumi 2:11 -14)(Luka 12:47). Mungu anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi gani k**a alivyo tayari kufuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje (Mathayo 12:42).
(6) KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.
Mmoja mmoja atasimama mbele ya kiti hicho kikubwa cheupe. Mahali hapo itakuwa mahali pa aibu na kudharauliwa (Daniel 12:2). Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa mfano wa Video iliyotunza kumbukumbu zake, Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi hapo (Ayubu 20:27)(Mithali 26:26)(Muhubiri 12:14)(Mathayo 10:26 -28)(1 Wakoritho 4:5)(Warumi 2:16). Mahili hapo tutawaona wahubiri wazinzi. Kila kitu kitaonyeshwa waziwazi. Hatua zote za mtu za kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kuingia naye nyumba ya kulal wageni na kufanya uchafu wote vyote vitaoneshwa mbele ya wote. Maneno yote ya mtu anayoyatamka yatawekwa wazi hapo na kwa kila neno mtu atahukumiwa (Mathayo 12:36-37). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya Injili bila kukata shauri na kuokolewa atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na wakati akirudi nyumbani atajiona anasema, “Siwezi kuokoka” wale walioshindwa kufanya hili au lile kwa visingizio kuwa ni wanajeshi, ni vijana wadogo n.k watawaona mashahidi wa Mungu waliofanya waliyoyakataa wakiwa na hali zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila kitu na kuwa mashahidi wa Mungu (Waebrania 12:1)(Mathayo 12:42)(Malaki 3:18;4:1-2).
(7) HUKUMU YA MWISHO.
Watu watajitetea kwa kilio na kusema “Mimi nilifanya miujiza kwa jina lako “Mimi nilitoa pepo kwa jina lako” watajitetea Mimi nilishuhudia na kufuatilia n.k. na Yesu atasema; Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu (Mathayo 7:22-23). Kila mtu atatolewa hapo na kuk**atwa kwa nguvu kasha atatupwa kwenye “ZIWA LA MOTO” Ziwa la moto ni tofauti na kuzimu au Jehanamu. Ziwa la mto kwa sasa halina mtu yeyote ndani yake, wa kwanza kutupwa humo watakuwa mnyama au Mpinga Kristo na Nabii wa uongo hilo litafanyika baada ya vita vya har-magedoni kabla ya utawala wamiaka 1,000 wa Yesu na watakatifu wake (Ufunuo 19:20). Kasha atafuata Shetani baada ya vita vya Gogu na magogu mwishoni wa utawala wa miaka 1,000 (Ufunuo 20:10). Mateso ya ziwa la mto ni mazito zaidi kuliko Jehanamu na moto. Mauti au kifo na Jehanamu ya sasa, vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote (Ufunuo 20:14 -15;21:18). Hapo itakuwa “KWAHERI YA KUTOKUONANA TENA” kwa wenye dhambi na watakatifu, HERI MWENYE SIKIO NA ALISIKIE NENO ROHO ANALIAMBIA KANISA.
Share this:
TwitterFacebook

Related
Ukiota unafanya mapenzi ndotoni maana yake una jini mahaba au jini maimuna.
January 4, 2021
With 3 comments
KUSIFU NA KUABUDU.
March 3, 2021
Ndoa Ya Serikali Ni Halali?
January 12, 2021
In "yesu"

Published by Peter Ogast
Servant of God!! View all posts by Peter Ogast

Post navigation
PREVIOUS
Previous post:BIBLIA INASEMA NINI JUU YA KUBET/BETTING,K**ARI,NA BAHATI NA SIBU?
NEXT
Next post:VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.
LEAVE A REPLY
Your email address will not be published. Required fields are marked *

Comment

Name *

Email *

Website

Notify me of new comments via email.

Notify me of new posts via email.

SEARCH
Search for:
Search
Search
MY LOGO

Advertisements

Address

Kariakoo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WATU WA MUNGU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to WATU WA MUNGU:

Share

Category