24/04/2026
1. Anamzungumzia ex wake mara kwa mara
Hata kwenye mazungumzo yasiyo na ulazima, jina lake linaibuka—inaonyesha bado yuko kichwani.
2. Anaficha mawasiliano yake
Anakuwa makini sana na simu, message au calls—kuna kitu hataki ujue.
3. Analinganisha wewe na yeye wa zamani
Maneno k**a “yule alikuwa hivi…” yanaonyesha bado anamkumbuka kwa undani.
4. Hajafunga ukurasa wa kumbukumbu
Bado ana picha, chats au vitu vinavyomkumbusha—na havionekani k**a anataka kuachia.
5. Hatoi 100% kwenye uhusiano wenu
Unahisi kuna pengo—upo naye, lakini si kwa moyo wote.