thony_tz

thony_tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from thony_tz, Kigoma.

"Siku ile niliyokuita uliniitikia, ukanifariji na kunitia Nguvu"Asante Mungu kwa maisha ya Castus de Anthony kiukweli am...
02/05/2025

"Siku ile niliyokuita uliniitikia, ukanifariji na kunitia Nguvu"
Asante Mungu kwa maisha ya Castus de Anthony kiukweli amefanyika Baraka kwetu ....
Naomba neema Yako ikawe juu yake akue akikupendeza wewe, Mjalie afya njema, Hekima, Utu wema, upendo na kuwajali wengine...
Awe mvumilivu na mstahimilivu....
Upole na hasira kwa kiasi....Amina🙏
HAPPY BIRTHDAY CASTUS de Anthony

Leo Papa Francis amezikwa katika Basilica la Santa Maria Maggiore lililopo Roma. Ni mazishi makubwa yaliyokusanya watu z...
26/04/2025

Leo Papa Francis amezikwa katika Basilica la Santa Maria Maggiore lililopo Roma. Ni mazishi makubwa yaliyokusanya watu zaidi ya laki mbili pamoja, huku mamilioni wakifuatilia kwa njia ya mtandao. Marais 50, Wafalme 10, wawakilishi wa wakuu wa nchi 130, viongozi wastaafu na wakuu wa mashirika ya kimataifa ni baadhi tu ya waliohudhuria Mazishi.

Papa Francis alifariki tarehe 21 April 2025. Siku k**a hii mwaka 1073 alifariki Papa Alexander II ambaye jina la kuzaliwa aliitwa Anselm da Baggio. Papa Francis amezikwa leo April 26 siku ambayo Papa Stefano II alifariki mwaka 757.

Papa Fransis amezikwa katika Basilica la Santa Maria Maggiore (picha ya pili) lililopo nje ya Vatican, tofauti na Mapapa wengi ambao wamezikwa katika Basilica Kuu la Mtakatifu Petro lililopo Vatican. Hata hivyo Papa Francis sio Papa wa kwanza kuzikwa ndani ya Basilica hili k**a ambavyo vyombo vingi vya habari vimeripoti. Kuna jumla ya Mapapa 7 waliozikwa hapa.

1. Papa Clement VIII alizikwa hapa 3 March 1605 jina lake la kuzaliwa aliitwa Ippolito Aldobrandini.

2. Pope Clement IX alizikwa hapa 9 December 1669 jina lake la kuzaliwa aliitwa Giulio Rospigliosi.

3. Papa Honorius III alizikwa hapa 18 March 1227 jina lake la kuzaliwa aliitwa Cencio Savelli.

4. Papa Nicholas IV alizikwa hapa 4 April 1292 jina lake la kuzaliwa aliitwa Girolamo Masci.

5. Papa Paul V alizikwa hapa 28 January 1621 jina lake la kuzaliwa aliitwa Camillo Borghese.

6. Papa Pius V alizikwa hapa 1 May 1572 jina lake la kuzaliwa aliitwa Antonio Ghislieri.

7. Papa Sixtus V alizikwa hapa 27 August 1590 jina lake la kuzaliwa aliitwa Felice Piergentile.

Papa wa mwisho kuzikwa nje ya Basilica kuu la Mtakatifu Petro kabla ya Papa Francis ni Papa Leo XIII. Huyu alizikwa mara mbili. Mara ya kwanza alizikwa Vatican ndani ya Basilica kuu la Mtakatifu Petro mwaka 1903. Lakini mwaka 1924 mabaki ya mwili wake yalihamishwa na kwenda kuzikwa nje ya Vatican, katika Basilica kuu la St.John Lateran, Roma.

Baada ya hapo Mapapa waliofuata wamekuwa wakizikwa Vatican ndani ya Basilica kuu la Mtakatifu Petro hadi leo ambapo Papa Francis amezikwa nje ya Vatican katika Basilica la Santa Maria Maggiore lililopo Roma.!
__
Credits: Polycarp Mdemu

🚨 BREAKING : PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIAKadinali Kevin Ferrel wa Vatican ametangaza kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa katoliki...
21/04/2025

🚨 BREAKING : PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA
Kadinali Kevin Ferrel wa Vatican ametangaza kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa katoliki Duniani Papa Francis amefariki Dunia leo asubuhi saa 1:35 alipokuwa kwenye makazi yake ya Kipapa huko Vatican.

Kiongozi huyo alikuwa kwenye mdororo mkubwa wa kiafya na ni jana tu ametoka kutoa salamu fupi za pasaka akinukuliwa “Hatujaumbiwa mauti Bali uzima” amefariki baada ya maradhi ya muda mrefu.

Raha ya Milele Umpe Ee Bwana!
Na mwanga wa milele umuangazie...
Apumzike kwa amani...Amina

Wydad Casablanca inaripotiwa kuwa wanatuma ofa ya pili kwenda Yanga SC kesho kwa ajili ya kuwashawishi wamuachie Mshambu...
22/08/2024

Wydad Casablanca inaripotiwa kuwa wanatuma ofa ya pili kwenda Yanga SC kesho kwa ajili ya kuwashawishi wamuachie Mshambuliaji wao Clement Mzize.

Awali Wydad walituma ofa ya USD 100,000 kwenda Yanga SC lakini dau hilo lilikataliwa.

Club ya Simba imetangaza rasmi kuwa Saido Ntibazonkiza Raia wa Burundi hatokuwa tena sehemu ya kikosi chao kwa msimu 202...
18/06/2024

Club ya Simba imetangaza rasmi kuwa Saido Ntibazonkiza Raia wa Burundi hatokuwa tena sehemu ya kikosi chao kwa msimu 2024/2025.

Simba wamefikia makubaliano ya kutokumuongezea mkataba baada ya mkataba wake wa awali kumalizika msimu ulioisha.

.......🚨|   *MICHUANO MIKUBWA BARANI ULAYA  NA WACHEZAJI WENYE ASILI YA AFRICA* 🌍 🚨🌍⤵️  Wachezaji katika kikosi cha Denm...
16/06/2024

.......🚨| *MICHUANO MIKUBWA BARANI ULAYA NA WACHEZAJI WENYE ASILI YA AFRICA* 🌍

🚨🌍⤵️ Wachezaji katika kikosi cha Denmark cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Yussuf Poulsen - Tanzania 🇹🇿

Alexander Bah - Gambia 🇬🇲

🚨⤵️ Wachezaji katika kikosi cha Austria cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Kevin Danso - Ghana 🇬🇭

Phillipp Mwene - Kenya 🇰🇪

🚨⤵️ Wachezaji katika kikosi cha Uhispania cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Nico Williams - Ghana 🇬🇭

Lamine Yamal - Morocco 🇲🇦

🚨⤵️Wachezaji wa kikosi cha Italia Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Michael Folorunsho - Nigeria 🇳🇬

Stephan El Shaarawy - Misri 🇪🇬

🚨⤵️Wachezaji sita katika kikosi cha England cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Bukayo Saka - Nigeria 🇳🇬
Kobbie Mainoo - Ghana 🇬🇭
Eberechi Eze - Nigeria 🇳🇬
Marc Guéhi - Cote d'Ivoire 🇨🇮
Ezri Konsa - DR Congo 🇨🇩
Joe Gomez - Gambia 🇬🇲

🚨⤵️Wachezaji wa tano katika kikosi cha Ujerumani cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Antonio Rüdiger — Sierra Leone 🇸🇱
Jamal Musiala — Nigeria 🇳🇬
Jonathan Glao Tah — Ivory Coast 🇨🇮
Benjamin Paa Kwesi Henrichs — Ghana 🇬🇭
Leroy Aziz Sané — Senegal 🇸🇳

🚨⤵️Wachezaji wanne katika kikosi cha Ureno cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Nélson Cabral Semedo — Cape Verde 🇨🇻
Danilo Pereira — Guinea 🇬🇳
Nuno Tavares Mendes — Angola 🇦🇴
Rafael Leão — Angola na São Tomé 🇦🇴 🇸🇹

🚨⤵️Wachezaji kumi na tatu katika kikosi cha Ufaransa cha Euro 2024 wana asili ya Kiafrika.

Brice Samba - DR Congo 🇨🇩
Ferland Mendy - 🇸🇳 Senegal & Guinea 🇬🇼
Dayot Upamecano - Guinea-Bissau 🇬🇼
Jules Koundé - Benin 🇧🇯
William Saliba - Cameroon 🇨🇲
Ibrahima Konaté - Mali 🇲🇱
Eduardo Camavinga - DR Congo 🇦🇴
Aurélien Tchouameni - Cameroon 🇨🇲
N'Golo Kanté - Mali 🇲🇱
Youssouf Fofana - Mali 🇲🇱
Mbappé - Cameroon 🇨🇲 & Algeria 🇩🇿
Dembélé - Mauritania 🇲🇷 & Mali 🇲🇱
Kolo Muani - DR Congo 🇨🇩
Bradley Barcola - Togo 🇹🇬

UPIGAJI SERENGETI WAMSH*TUA WAZIRI MKUU ACHUKUA HATUA KALISerengeti Media Centre Waziri Kassim Majaliwa amemwagiza Kaman...
28/02/2024

UPIGAJI SERENGETI WAMSH*TUA WAZIRI MKUU ACHUKUA HATUA KALI

Serengeti Media Centre

Waziri Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase kumk**ata Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti,

Saad Mutunzi Ishabailu kwa kosa la kuhamisha sh. 213,748,085 kwa awamu nne kwa njia ya uhamisho wa ndani kwa kushirikiana na watumishi wa TAMISEMI na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

Ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwenye kikao kilichofanyika katika kwenye Halmashauri hiyo, mkoani Mara.

Waziri Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kuwaeleza watumishi na madiwani mbinu wanazotumia watumishi wachache wa baadhi ya Halmashauri ambao walikuwa wanashirikiana na watumishi watatu wa kitengo cha Treasury Single Account (TSA) kuiba fedha za umma.

Akitolea mfano juu ya mbinu zinazotumika na wachache hao, Waziri Mkuu aliwaeleza watumishi wa Halmashauri hiyo pamoja na Madiwani kwamba Juni 10, 2023 walitumia mwanya wa kuombea kibali fedha za bakaa kwa barua iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Chatta Luleka.

Amesema Juni 21, mwaka jana Bw. Ishabailu alianza kufanya matumizi ya hizo fedha kwa kushirikiana na mfanyabiashara wa hapa Mugumu, Bw. Daudi Matinde Chacha kupitia kwenye akaunti zake za NMB na CRDB kwa kupitia miamala minne ya sh. milioni 76.3, sh. milioni 57.7, sh. milioni 47 na sh.milioni 32.5.

Amesema alipoulizwa na timu ya uchunguzi Matinde alikiri kuwa haidai fedha yoyote Halmashauri ya Serengeti isipokuwa mweka hazina huyo aliomba apitishie fedha zake kwenye akaunti zake kwa sababu zinahitajika haraka kwa matumizi ya ofisi. “Aliambiwa atoe shilingi milioni 189 akamkabidhi zote Ishabailu na zilizobakia (sh. milioni 24) akaambiwa abaki nazo,” amesema Waziri Mkuu.

Aliwasisitiza madiwani na watumishi kuwa makini na matumizi ya fedha za umma kwani serikali inapotafuta fedha na kuzileta kwenye Halmashauri zinatakuwa kutatua kero za wananchi walio wengi.

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Jovitus Francis Mwijage (mbele) akiwa amekaa katika Kiti cha Kiaskofu muda mfup...
27/01/2024

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Jovitus Francis Mwijage (mbele) akiwa amekaa katika Kiti cha Kiaskofu muda mfupi baada ya Kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo.

TUMUOMBE ILI AWEZE KUIFANYA KAZI ALIYO KABIDHIWA YA KULICHUNGA KUNDI LA MUNGU.

Mungu hajawahi kushindwa......!Mpaka sasa nasema asante Mungu kwa kunishindia kifo kilichokuwa mbele yangu.....Mpaka nim...
05/12/2023

Mungu hajawahi kushindwa......!
Mpaka sasa nasema asante Mungu kwa kunishindia kifo kilichokuwa mbele yangu.....
Mpaka nimeweza kufika shambani na kupanda Karanga na maharage Dah...
Sina neno kwako Mungu.
"Mungu akisema ndio hakuna wa kupinga"
Asanteni sana ndugu jamaa na marafiki mlionipambania kwa hali na mali pamoja na maombi yenu sitachoka kuwashukuru kiukweli ni ngumu kumtaja kila mmoja ila natamani ningeweza mmenifanya nione duniani siko mwenyewe.
"Ishi na watu kula na watu" Msemo wa mzee wangu alipenda sana kuutaja hasa akiwa kapiga soda mweleka ndio nimeiona maana halisi baada ya janga lililonikuta nilivoishi na kula na watu hao ndio walioniokoa nikiwa na matatizo.
All in all asanteni sana ndugu zangu



Moyo unahitaji muda zaidi kukubali kile ambacho akili imeshajua, Tena inakuwa ngumu kulala wakati Moyo unapigana vita na...
26/09/2023

Moyo unahitaji muda zaidi kukubali kile ambacho akili imeshajua, Tena inakuwa ngumu kulala wakati Moyo unapigana vita na Akili.
Muombe Mungu Sana Vita hiyo iwe ya kuleta Amani na furaha.

Address

Kigoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when thony_tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share