Philipo Mella

Philipo Mella Sports and Entertainment

19/04/2023

Hallelujah

๐—ฅ๐—ฎ๐—ถ๐˜€ ๐˜„๐—ฎ ๐—–๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—ซ๐—ถ ๐—๐—ถ๐—ป๐—ด ๐—ฃ๐—ถ๐—ป๐—ด  ๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚๐—น๐—ถ๐—ฎ. Nikiwa mtoto mdogo, nilikuwa ๐—บ๐—ฏ๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐—ณ๐˜€๐—ถ sana, kila mara nilipenda kujinyakulia kil...
21/01/2023

๐—ฅ๐—ฎ๐—ถ๐˜€ ๐˜„๐—ฎ ๐—–๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—ซ๐—ถ ๐—๐—ถ๐—ป๐—ด ๐—ฃ๐—ถ๐—ป๐—ด ๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚๐—น๐—ถ๐—ฎ.



Nikiwa mtoto mdogo, nilikuwa ๐—บ๐—ฏ๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐—ณ๐˜€๐—ถ sana, kila mara nilipenda kujinyakulia kilicho bora zaidi.

Polepole, kila mtu aliniacha na sikuwa na marafiki. Sikuona k**a hilo lilikuwa ni kosa langu badala yake niliishia kuwakosoa wengine.

Lakini baba yangu alinipa darasa la kunisaidia maishani.

Siku moja, baba yangu alipika bakuli 2 za tambi(noodles) na kuziweka juu ya meza. Moja lilikuwa na yai juu huku bakuli lingine halina hata yai moja juu.

Kisha akanitaka nichague bakuli moja.

Kwa sababu mayai yalikuwa adimu siku hizo, nilichagua bakuli lenye yai!

Nilikuwa najipongeza kwa uamuzi wangu wa busara wa kuchagua bakuli lenye yai. Kwa mshangao wangu, niliona kwamba bakuli la babangu lilikuwa na mayai mawili chini!

Kwa majuto mengi, nilijikaripia kwa kuwa na haraka katika uamuzi wangu.

Baba yangu alitabasamu, *๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ถ๐—ฎ, ๐˜€๐—ถ๐˜†๐—ผ ๐—ธ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ผ๐—ธ๐—ถ๐—ผna ๐—บ๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ถ ๐—ธ๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐˜‚๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—น๐—ถ.*

Aliongeza kuwa, *๐—จ๐—ธ๐—ถ๐—ท๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ฎ ๐˜๐—ฎ๐—ฏ๐—ถ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ท๐—ถ๐—ป๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ na kujipendelea ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐—ด๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ๐˜๐—ฎ ๐—ต๐—ฎ๐˜€๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ.*

Siku iliyofuata, baba yangu alipika tena bakuli 2 za noodles: bakuli moja na yai juu na bakuli lingine bila yai juu,na kuleta mezani.

Tena, alinitaka kuchagua bakuli nililotaka.

Wakati huu, nilihisi mjanja kwa hivyo nilichagua bakuli bila yai lolote juu.

Mmmmm kwa mshangao, hapakuwa na hata yai moja chini ya bakuli!

Tena baba alitabasamu na kuniambia, ๐—บ๐˜๐—ผ๐˜๐—ผ ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐˜‚, ๐˜‚๐˜€๐—ถ๐˜๐—ฒ๐—ด๐—ฒ๐—บ๐—ฒ๐—ฒ ๐˜‚๐˜‡๐—ผ๐—ฒ๐—ณ๐˜‚ ๐—ธ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜€๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ ๐—บ๐˜„๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ป๐—ฒ, ๐—บ๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ๐—ป๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฑ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—ฎ๐˜‚ ๐—ธ๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ถ๐—ฎ ๐—ต๐—ถ๐—น๐—ฎ.

๐—ž๐—ฎ๐—บ๐˜„๐—ฒ ๐˜‚๐˜€๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐˜€๐—ถr๐—ถ๐—ธ๐—ฒ ๐—ฎ๐˜‚ ๐—ธ๐˜‚๐—ต๐˜‚๐˜‡๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐˜€๐—ฎ๐—ป๐—ฎ, ๐˜‚๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ต๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ณ๐˜‚๐—น๐—ฎ๐—ป๐—ถ, ๐—ฐ๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—น๐—ถ๐—ฎ ๐˜๐˜‚ ๐˜‚๐˜‡๐—ผ๐—ฒ๐—ณ๐˜‚ ๐—ธa๐—บ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ ๐˜€๐—ผ๐—บ๐—ผ ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ผ ๐—ต๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ถ ๐—ธ๐˜‚p๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚ ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐˜ƒ๐˜†๐—ผ๐˜๐—ฒ ๐˜ƒ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—ฎ๐—ฑ๐—ฎ.

Siku ya tatu, baba yangu aliweka tena bakuli 2 za noodles, bakuli moja na yai juu na nyingine bila yai juu.

Alinitaka nichague bakuli nililotaka.

Lakini wakati huu, nilimwambia baba yangu, Baba, chagua kwanza. Wewe ndiye kichwa cha familia na unachangia zaidi kwa familia.

Baba yangu alifurahi sana na alinichagulia.

Alichagua bakuli lenye yai moja juu. Lakini nilipokuwa nikila bakuli langu la tambi, kwa mshangao wangu, kulikuwa na mayai mawili chini ya bakuli.

Baba yangu alitabasamu kwa upendo machoni pake. Alisema, ๐—บ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ด๐˜‚, ๐—ป๐—ถ ๐—น๐—ฎ๐˜‡๐—ถ๐—บ๐—ฎ ๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐˜‚๐—ธ๐—ฒ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐—ฝ๐—ผ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ฎ๐—ท๐—ถ๐—น๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ป๐—ฒ, ๐—บ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐—บa๐˜‡๐˜‚๐—ฟ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฒ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ธ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ.

Kupitia hii hadithi ya ๐—ซ๐—ถ ๐—๐—ถ๐—ป๐—ด ๐—ฃ๐—ถ๐—ป๐—ด, tunapoendelea na safari ya 2023 na mambo yetu yaende barabara.

โžก๏ธTunatakiwa tufikirie manufaa ya wengine ndipo mema yatakapotujia.

โžก๏ธKatika kutimiza malengo yetu, tusiwe wabinafsi; bali pia tunapaswa kutilia maanani mikakati ya wengine ili furaha yetu husika ikamilike.

โžก๏ธTusikimbilie nafasi, cheo, mali, umaarufu n.k kwa kuwaangusha,kuwadharirisha, kuwaangamiza au kuwaponda wengine ili tu kupata chochote tunachotaka.

*Mungu wa mbinguni azidi kutupa hekima, busara kila tunapoiwazia kesho yetu*

*NI MAMA AU NI MAMA YAKO*?*Salum alimtumia meseji mke wake; โ€œSamahani mke wangu sitaweza kuja kukuchukua, nipo Hospitali...
23/12/2022

*NI MAMA AU NI MAMA YAKO*?

*Salum alimtumia meseji mke wake; โ€œSamahani mke wangu sitaweza kuja kukuchukua, nipo Hospitalini hapa Mama amelazwa kapungukiwa damu ndiyo nahangaikia watu wa kumuongezeaโ€*

*Mkewe akajibu; Kwahiyo Mama yako ndiyo umemuona wa muhimu sana kuliko mimi, yaani mimi nipande Bajaji kisa Mama yako anaumwa, si umuache uje unichukue, unakaa huko kwani wewe Daktari!*

*Gari yangu mwenyewe kisha unisumbue sababu ya Mama yako! Umesikia gari ya wagonjwa hiyo, ungetaka kumhudumia Mama yako si ungenunua ya kwako!โ€*

*Salum alimuulizaโ€™; Kwahiyo ni muache Mama hapa nije kukuchukua?โ€ Mkewe alimjibu, ndiyo kwani ukimuacha atakufa! Si ushasema yuko hospitalini! Si kuna madaktari huko!*

*Nitaendaje kwenye sherehe peke yangu k**a vile sina mume!โ€ Salum alikata simu na baada ya k**a nusu saa hivi alikua nyumbani tayari kumchukua mkewe, kwahasira mke alipanda kwenye gari, walienda mpaka kwenye sherehe.*

Sherehe ilianza, huku mke akinywa kwa hasira hakutaka hata kuongea na mumewe.

Salum alikaa kimya akiwa na mawazo mengi kila mara akishikilia simu yake. Katika kipindi chote hicho mkewe hakumuuliza hata hali ya Mama.

Sherehe iliisha wote wakaingia kwenye gari kurudi nyumbani. Walilala mpaka asubuhi mkewe akiwa hajamuulizia chochote.

Asubuhi wakati wanaamka simu ya mwanamke ikatoa mlio Wa Meseji, ujumbe ulitumwa kutoka kwa Mdogo wake Wa tumbo moja ukasomeka hivi:

"Dada! mama amelazwa hospitali tangu Jana, tulimuona tu shemeji we we ulikua wapi?"

Ghafla uso ukabadilika akamgeukia Mume wake na kumuuliza "kumbe anaeumwa ni mama yangu! Mbona hukuniambia??

Salumu akajibu:

*โ€œJamani jana si nilikuambia anaumwa hali mbaya kalazwa hospitalini?โ€*
*โ€œUliniambia lakini hukuniambia k**a ni Mama yanguโ€*
*โ€œJamani mke wangu sisi ni mwili mmoja, sasa niliposema Mama nilikua na haja gani ya kusema Mama yangu au wako, kwamaana ninavyojua Mama yangu Mama yako na Mama yako ni Mama Yangu.*

*Huku akilia. โ€œSasa ndiyo ukamuacha Mama hospitalini, kwani kapatwa na nini? Yaani unanaicha na sherehekea kumbe Mama yangu anaumwa!โ€*

โ€œAlipata ajali ya gari jana, akapoteza damu nyingi, sasa hospitalini kulikua hakuna damu ndiyo nikawa natafuta watu wa kumuongezea, sema uliposema niache kuhangaika naye ndiyo nikaacha sasa sijui hali yake inaendeleaje maana alizidiwa sana".

Huku akilia mkewe aliingia kwenye gari kwa kasi akimtaka mumewe aendeshe gari kwa haraka, Salum aliendesha gari taratibu akipitia ofisini kwao kusaini, mkewe alilalamika kwamba wanachelewa

Kwa namna alivyokuwa amechanganyikiwa mkewe alishindwa hata kuendesha gari hivyo ilibidi amsubiri mumewe waondoke wote. Njia nzima mkewe alikua akilia.

Mkewe alijua Mama yake alishakufa kwa kukosa damu kwani kwa hali aliyoelezewa alijua kuwa hawezi pona. Alifika na kuwakuta ndugu zake wako nje, aliwasalimia na kuwauliza hali ya Mama walimuambia aingie kumuona.

Alizidi kuchanganyikiwa akijua Mama yake kashafariki.

Alifika na kumkuta Mama yake mzima, alimsalimia na kumuomba msamaha kwa kuchelewa kuja kumuona akisema alikua hajui, Mama yake alimuuliza kwa mshangao.

*โ€œUlikua hujui wakati Mumeo jana alikuwa hapa, Baba wa watu kahangaika sana mpaka kupata watu wa kuniongezea damu, kasumbuka sana jana, mwanangu hapa umepata mume. Asingekua mumeo ningeshakufa kwani madakitari walisema ningekosa damu ningekufaโ€ฆโ€*

Mke wa Salum alishindwa cha kujibu, hakujua kuwa kumbe Salum hakuacha kutafuta damu alihakikisha Mama yuko salama ndiyo akaondoka.

โ€œSikumwambia Mama, Jana alikua anajisikia vibaya, nadhani presha ilikua inamsumbua, nikasema nisimwambie kwani angeweza kuchanganyikiwa. Asubuhi ndiyo nikamuambia baada ya kuona yuko vizuriโ€

"Naendela vizuri mwanangu, ahsante sana kwa kuhangaika na mimi jana, nilikua hoi sana". Mama yake aliongea huku akitabasamu. Mkewe alinyanyuka, huku akitoa machozi alimkumbatia mumewe na kumwambia: "nisamehe mume wangu sasa ndiyo nimejua maana ya ndoa"

Salum alimkumbatia mkewe kwa nguvu na kumwambia.

"Usijali mke wangu nakupenda sana nilitaka tu ujifunze kuwa mali sio kila kitu, najua umenizidi kipato lakini pesa zinatafutwa na kamwe hela haiwezi kuzidi thamani ya utu"

*JIFUNZE KISHA Funza wengine*

Upendo udumu daimaโฃ๏ธโฃ๏ธโฃ๏ธ
22/12/2022

Upendo udumu daimaโฃ๏ธโฃ๏ธโฃ๏ธ

17/12/2022
๐Ÿ”ฐ ZA HIVI PUNDE ||โ€ข Simba imekamilisha usajili wa nyota watatu ambao ni ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‰Ceasor Manzoki,  ๐Ÿ‘‰Luis Miquissone ๐Ÿ‘‰Saido Ntib...
16/12/2022

๐Ÿ”ฐ ZA HIVI PUNDE ||โ€ข

Simba imekamilisha usajili wa nyota watatu ambao ni ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
๐Ÿ‘‰Ceasor Manzoki,
๐Ÿ‘‰Luis Miquissone
๐Ÿ‘‰Saido Ntibazonkiza

Wale wa kubisha daima endeleeni kubisha tu daima โœ”๏ธโœ”๏ธ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ”ฅ

09/10/2022

Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Acquaint now thyself with him, and be at peace: thereby good shall come unto thee.

Address

Iyunga
Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Philipo Mella posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Philipo Mella:

Share